Header Ads Widget

RC, DC, DED SHIRIKIANENI ,TIMU ZINAZOTEKELEZA MRADI WA UBORESHAJI USALAMA WA MILKI ZA ARDHI

NA HAMIDA RAMADHANI MATUKIO DAIMA AAP DODOMA

WAKUU wa Mikoa,Wakuu wa Wilaya na Wakurugenzi wa Halmashauri zinazotekeleza mradi wa kuboresha Usalama wa Milki za Ardhi wameagizwa kutoa ushirikano kwa timu zinazotekekeza Mradi huo zikiwemo taasisi zinazofanya kazi na mradi kama vile NIDA,NEMC, Tume ya Mipango ya Matumizi ya Ardhi, Vyuo vya Ardhi na Taasisi nyingine . 


Agizo hilo limetolewa Leo jijini hapa na Waziri wa Ardhi ,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Jerry Silaa wakati akiongea kwa niaba ya Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa kwenye mkutano wa kitaifa wa wadau kujadili utekekezaji wa Mradi huo ambapo amesisitiza ushirikiano wa kutosha katika utekelezaji wa mradi. 


Aidha, nawaagiza wakurugenzi wa Halmashaurii nchini katika kipindi cha maandalizi ya Bajeti ya mwaka 2024/25 watenge fedha kwa ajili ya sekta ya ardhi ili kuendeleza utekelezaji wa mradi katika maeneo yale ambayo mradi haujaweza kufika.

Vilevile, amewataka watalaam wa sekta ya ardhi washirikiane na viongozi wa Serikali za mitaa na vijiji kuwapa wananchi elimu kuhusu masuala ya ardhi na hususan taarifa za utekelezaji wa mradi huo. 


"Napenda kuipongeza Wizara kwa mradi huu mkubwa zaidi wa ardhi chini ya Jangwa la Sahara unaofadhiliwa na Benki ya Dunia, " Amesema


Amesema Wizara kwa kushirikiana na Wizara ya Fedha ihakikishe katika kutekeleza mradi huu sheria na taratibu za nchi pamoja na miongozo ya Benki ya Dunia vinazingatiwa katika kusimamia mradi huu. 


"Kwa niaba ya Serikali 

kuishukuru Benki ya Dunia na wadau wengine wa maendeleo kwa juhudi kubwa wanazofanya kuhakikisha ustawi wa Taifa letu na wananchi wake, " Amesema 


Hata hivyo amewahakikishia kuwa Serikali itasimamia miradi hii kikamilifu ili kufikia malengo tarajiwa.

Pia amesema tarehe 21 Januari 2022 Serikali kupitia Wizara ya Ardhi, Nyumba 

na Maendeleo ya Makazi ilisaini makubaliano na Benki ya Dunia ya mkopo wa Shilingi bilioni 346 sawa na dola za kimarekani milioni 150 kwa ajili ya utekelezaji wa Mradi wa Kuboresha Usalama wa Miliki za Ardhi nchini. 


"Mradi huu unatekelezwa 

katika kipindi cha miaka mitano (5) na una vipengele vinne (4) ambavyo ni Kuongeza Usalama wa Milki; Kuimarisha Mifumo ya Taarifa za Ardhi; Kujenga Miundombinu ya Ardhi na Usimamizi wa Mradi ambapo Mradi huu utatoa fursa mbalimbali katika makundi,"Amesema Waziri Slaa

Kwa upande wake Katibu Mkuu Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi Anthony Sanga amesema Kupitia zoezi hilo, jumla ya Tsh. 270,255,481/= zimekusanywa kama maduhuli ya Serikali yatokanayo na ardhi katika kipindi cha kuanzia Septemba 2023 hadi sasa.


Mradi umelenga kujenga ofisi za ardhi za mikoa 25 ambazo zitazingatia mahitaji ya mfumo unaojengwa wa kielektroniki wa usimamizi wa ardhi nchini. 


Amesema Ujenzi huu pia unakwenda sambasamba na ujenzi wa madarasa (lecture theatres) mawili katika Chuo cha Ardhi Tabora na mawili katika Chuo cha Ardhi Morogoro ukamilishaji wa zabuni za ujenzi  upo katika hatua za mwisho.


"Mradi umeendelea kusaidia kuboresha Mabaraza ya Ardhi ili kuongeza ufanisi katika kutatua migogoro na kesi mbalimbali za ardhi ambapo Katika hatua hiyo mradi umewezesha kupunguza mlundikano wa kesi ambapo mashauri 458 tayari yamefanyiwa kazi katika mabaraza matano (5) ndani ya kipindi cha takriban mwezi mmoja, "Amesema Katibu Mkuu Sanga

Pia, mradi umetoa samani za ofisi na vitendea kazi kwa baadhi ya mabaraza ikiwa ni sehemu ya kuboresha mazingira ya kufanyia kazi.


Mradi uliazimia kujenga vituo 22 vya kielektroniki vya upimaji (Continuous Operationg Reference Station CORS), miundombinu inayoendana na CORS, na kuweka alama mpya za msingi 400 za upimaji ardhi katika Halmashauri 34 Tanzania Bara ambapo hatua za kumpata mjenzi na mtaalam mwelekezi zipo zinaendelea. 


Aidha, alama hizo zitawezesha na kurahisisha shughuli mbali mbali za upimaji wa ardhi nchini ikiwemo upimaji wa maeneo yaliyotengwa kwa ajili ya urasimishaji  Mpaka sasa mradi umeweka jumla ya alama mpya za upimaji 197 kati ya alama 400 zinazotarajiwa kuwekwa katika Halmashauri 14 kati ya Halmashauri 38 nchini Hii ni sawa na asilimia 49% ya malengo ya mradi.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI