Header Ads Widget

WAZIRI UMMY MWALIMU : SERIKALI ITAENDELEA KUWAWEZESHA WATAALAMU WA AFYA KUPATA UJUZI NJE YA NCHI

 

 (Matukio Daima)

Waziri Ummy Mwalimu amesema kuwa Serikali itaendelea kuwawekea mazingira rafiki madaktari na wahudumu wengine wa afya kwenye wa Taasisi ya Tiba ya Mifupa na Ubongo Muhimbili (MOI) pamoja na kwenye hospitali nyingine ili kwenda kupata ujuzi na ubabobezi nje ya Nchi ambao utakuja kuleta tija kwa Nchi.


Akizungumza katika uzinduzi wa miundombinu mbalimbali kwenye taasisi ya MOI leo tarehe 28, 2023 amesema kuwa Serikali imekuwa ikitenga pesa kwa ajili ya kuwawezesha wataalamu mbalimbali wa Afya kwenda kuongeza ujuzi zaidi, ameelekeza Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya MOI Prof. Charles Mkony kuandaa utaratibu kwa wataalamu ambao wanaweza kunufaika na utaratibu huo.


Waziri Ummy pia ameipongeza taasisi ya MOI kwa kuanzisha mradi wa kliniki mpya ya wagonjwa maalumu wa kimataifa (premier and international service) ambapo amesema kuwa mradi huo unaenda kuwezesha huduma za moja kwa moja kwa wagonjwa maalum ambao wamekuwa wakifuata mazingira ya huduma za aina hiyo nje ya Nchi.


Aidha amewahasa kuendelea kuboresha huduma hizo ikiwemo huduma za mapokezi kwa wagonjwa wanaotokea nje ya Nchi, ambapo amesema kuwa huduma hizo zikiwa rafiki zitaendelea kuvutia watu.

Hata hivyo amewahasa kutunza vyema kumbukumbu za wangonjwa wanaotokea nje ya Nchi ambao wamekuwa wakitumia baadhi ya hospitali za ndani. Ambapo amedai kuwa kumbukumbu zitasaidia katika kufanya tathimini mbalimbali.


Amesema kuwa kwa siku za hivi karibuni wagonjwa kutokea nje ya Nchi wamekuwa wakija kwenye hospitali za ndani kupatiwa huduma jambo ambalo linaleta faida za kiuchumi.


Mwenyekiti Bodi ya Wadhamini wa Taasisi ya MOI Prof. Charles Mkony ameomba Serikali kupitia Waziri wa Afya, Ummy Mwalimu kuwawekea mazingira rafiki ya kimapato wahudumu kwenye hospitali hiyo ambao wamekuwa wakitekeleza majukumu nyeti ambapo wahudumu wa aina hiyo wapo wachache.

Sanjari na hilo Mwenyekiti huyo ametoa wito kwa Serikali kuteua wajumbe wa Bodi ambao wamekosekana kwa zaidi ya mwaka mmoja.


Pia mdau wa Damu salama, Azim Dewji ambaye amekuwa akishiriki katika masuala mbalimbali ya sekta ya afya ikiwemo kwenye taasisi ya MOI ametoa wito kwa wadau wa michezo ikiwemo Simba na Yanga kuona umuhimu kushikana na taasisi ya MOI katika masuala mbalimbali yanayolenga kuwasaidia wananchi wahitaji wa huduma, hususani katika zoezi la kuchangia damu salama pamoja na fedha tasrimu ili kusaidia wahitaji.


Waziri Ummy Mwalimu amezindua miradi na miundombinu mipya ambayo ni, mradi wa kliniki mpya ya wagonjwa maalumu wa kimataifa (premier and international service), eneo la wateja kusubiria huduma katika eneo la EMD (MOI Clients' lounge), Uzinduzi wa Mashine mpya za MRI, uzinduzi wa Mashine mpya za CT SCAN , uzinduzi wa miongozo standard operating procedures (SOPS) na MOI Hospital Formula.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI