Header Ads Widget

KAMPUNI YA SANAI YAIOMBA SERIKALI KUWASAIDIA KUPATA HAKI YAO

Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 

Kampuni inayojishughulisha na uuzaji wa vifaa tiba Sanai Medical Supply imeifungulia kesi ya madai ya kujipatia mali kwa njia ya udanganyifu kampuni ya Afrika Inland Logistic Limitted.


Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Kampuni hiyo, Juma Seleman Sanai mara baada ya kutoka kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam amesema wanaidai kampuni hiyo zaidi ya sh. milioni 100.


Aidha, ameiomba Serikali kuwasaidia kuweza kupata haki yao ambayo wanaidai kampuni hiyo kwa miezi mitano sasa ambapo wamefatilia madai hayo kwa miezi 2 bila ya mafanikio yoyote hali iliyopelekea kwenda kuripoti kituo cha Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

 

"Tumepata taarifa kuwa ifikapo Desemba 1, 2023 kampuni mpya itaingia na wao kuondoka hivyo tutakosa wa kumdai na ndio maana wanatuzungusha hivyo tumekuja kuripoti Polisi Ili Serikali itusaidie sisi wazawa ambao tunataka kutapeliwa na kampuni hiyo ya wahindi” amesema Mkurugenzi Sanai.

Hata hivyo ameiomba Serikali kuhakikisha wao kama wawekezaji wazawa wanapatiwa haki zao na hatua zichukuliwe Kwa kampuni kuanzia uhalali wake wa kufanya kazi hapa nchini.


"Sisi tumefanya kazi Kwa muda mrefu na Kampuni hii bila vikwazo ila toka umeingia uongozi Mpya akiwemo mhasibu Dinesh wamekuwa wakitusumbua sana kwenye malipo pindi tunapofika kudai fedha zetu ambapo hadi sasa imefikia zaidi ya Milioni 160 kutokana na makubaliano ya mkataba kuwa ucheleweshwaji wa malipo Kwa mwezi mmoja kutaongezeka kiwa Cha Fedha Kwa asilimia 23" ameongeza Mkurugenzi Sanai.


Mtandao wa Matukio Daima baada ya kupata taarifa hiyo uliamua hadi kufika kituo cha Polisi Kanda maalum ya Dar es Salaam kwa ajili ya kufutialia tukio hili kwa ukaribu.


Matukio Daima ilifanikiwa kuzungumza na Kaimu Kamanda wa kanda maalum ya Dar es Salaam ACP Gabriel Pupa kwa njia ya simu ambapo amesema kuwa ni kweli kuwa malalamiko hayo yameripotiwa kituoni hapo Novemba 27/2023.


Aidha amesema walalamikiwa waliitwa Novemba 28/2023 na kuhojiwa na kitengo Cha upelelezi ambapo Novemba 29/2023 mlalamikaji na mlalamikiwa walifika kituoni hapo na kukubaliana kulipa fedha hiyo kabla hawajaondoka nchini.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI