NA FRANCIS GODWIN , IRINGA
MAHAKAMA zimeshauriwa kabla ya kutoa maamuzi yake ya mwisho hasa kwa mwanamke kukuangalia sababu juu ya sababu ya mwanamke kufanya kosa ndipo itoe hukumu kwa matakwa na kwa mujibu wa sheria kuangalia mahitaji ya marekebisho ya yule unayemtia hatiani .
Kuwa hata katika misingi ya viwango vya kimataifa vinasema unapotaka kumtia hatiani mtu aliyekosa inataka kuangalia hitaji ya marekebisho kwa huyu anayetakiwa kupewa adhabu kabla ya kumpa adha ili adhabu iwe kumrekebisha kuwa mtu mwema katika jamii.
Akizungumza katika mahojiano maalumu na Matukio Daima Media jana ofisini kwake afisa uangalizi mfadhiwi wa mkoa wa Iringa Hamis Jengela alisema kuwa ofisi yake inashughulika na utekelezaji wa adhabu mbadala wa kifungo gerezani alisema kuwa kuwa pamoja na kuwa uwezo wa ofisi yake ni mfungwa aliyefungwa kifungo cha miaka isiyo zidi mitatu ndio ambao wanaweza kumsaidia kupata adhabu mbadala na sio aliyefungwa zaidi ya miaka mitatu kama ilivyo kwa kesi ya Maria Ngoda aliyefungwa miaka 22 kwa kosa la kukutwa nyara za serikali ambayo ni nyama ya swala vipande 12.
Alisema kuwa hadi sasa ofisi yake haijapata kumsaidia mfungwa aliyefungwa miaka kama hiyo ya Maria Ngoda japo alisema wamepata kuwasaidia wafungwa ambao walifungwa kwa makosa ya kuua bila kukusudia na wengine ambao walihukumiwa kwa makosa ya kuingia Hifadhini kinyume na sheria .
Kuwa ili kupata msaada wa huduma za kijamii ni lazima ombi litoke gerezani kwa mkuu wa gereza na ofisi yake inakwenda kufanya uchunguzi kwenye jamii ili kujua kama kuna madhara yoyote ya mhusika iwapo atapewa adhabu mbadala .
Jengela alisema kuwa mahakama inapaswa kuangalia sana kabla ya kumtia hatiani mtu anayekosa kuangalia hitaji la marekebisho ila wakati mwingine mahakama zetu hazifikirii sana katika kutoa adhabu kwa wakosaji .
“Ni sahihi sana inapofika hatua ya kutoa adhabu kufikiri sana ili kuangalia adhabu sahihi ambayo itakuwa hailengi ukubwa wa kosa ila inalenga kumrekebisha mtu kuwa raia mwema na sio kumkomesha “
Akijibu swali la mwandishi juu ya mtazamo wa wengi juu ya kesi ya malkia ya pembe za Ndovu aliyekutwa na vipande 511 vya meno ya Tembo kupigwa faini alisema kuwa hapo ndipo anajikuta akijiuliza kwa mahakama ya Kisutu iliyompiga faini malkia wa vipande 511 vya meno ya Tembo ilitazama nini na mahakama ya Iringa iliyomfunga Maria Ngoda kwa kukutwa na nyama ya swala vipande 12 iliangalia nini .
Alisema kuwa wakati mwingine mahakama inapofika hatua ya mwisho kuangalia mahitaji ya marekebischo ya mtu unayemtia hatiani .
Hata hivyo alisema kuwa wakati mwingine kwenye utekelezaji wa sheria na maamuzi huwa na mitazamo tofauti kwa watoa haki japo asingependa kushutumu mahakama zote kwani ni vema kuangalia kwa kina mahakama ya Kisuti iliangalia nini na mahakama ya Iringa ilitazama nini kwani sheria inanalenga kuadhibu ,kumrekebisha ama kumuonya mkosaji hivyo vyete vinawezekana .
Alisema kuwa kumekuwa na mitazamo tofauti kati ya kesi ya pembe za Ndovu 511 na adhabu iliyotolewa na nyama ya Swala vipande 12 kuwa na adhabu kubwa zaidi .
Aidha alisema kuwa toka amekuwepo katika ofisi hiyo amejifunza kuwa kuwa sehemu sheria imekaa vema na sehemu sheria hiyo hapo vizuri ila kwa upande wa kulinda raslimali za Taifa anaona sheria imekaa vizuri na vema jamii kuepuka kufanya makosa ya ujangili .
Pia alisema bunge limetunga sheria nzuri ya ujangili na uhujumu uchumi ila watendaji wa mahakama wanayo nafasi ya kuboresha sheria za bunge Kwenda vema zaidi na kuwa watendaji ni sehemu ya sekretarieti ya serilkali lazima kufanya kazi ya kuisaidia serikali na kufanya kazi kwa weledi zaidi .
Alisema kuwa suala la kupewa adhabu mbadala kwa mfungwa na adhabu kama adhabu nyingine kwani bado utakuwa mfungwa isipo kuwa utakuwa mfugwa huku ukihudumia familia yako .
Sakata la Mjane Maria Ngoda limeendelea kuchukua sura mpya kwa jamii kuonesha nia ya kumsaidia mjane huyo na tayari umoja wa wanawake Tanzania (UWT) kupitia mwenyekiti wake Mary Chatanda imejitokeza kutaka kumsaidia mjane huyo kumwekea wanasheria ili kusaidia kumkatia rufaa.
Katibu Mwenezi wa chama cha mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Joseph Lyata alisema kuwa CCM mkoa wa Iringa wamejinga kufuatilia familia yam jane huyo ili kuona namna ya kuisaidia na kama inazo sifa za kuwepo kwenye mpango wa kunusuru kaya masikini Tanzania (TASAF) basi kuingizwa katika mpango huo na pia kujua sababu za mtoto wa mjane huyo kukatisha masomo ya sekondari na ikiwezekana kumsaidia kuendelea na masomo ya sekondari.
Chama cha mawakili Tanganyika (TLS ) mkoa wa Iringa kimejitokeza kumsaidia mjane huyo pasipo gharama kwa kupanga jumla ya mawakili 10 ambao watafanya kazi ya kumtetea mjane huyo mahakamani .
Mwenyekiti wa TLS mkoa wa Iringa Moses Ambindwile alisema idadi ya mawakili imeendelea kuongezaka na kuwa kuna uwezekano wa mawakili kuongezaka zaidi na lengo la TLS kuona mjane huyo anasaidia msaada wa kisheria na kuwa leo Ijumaa watawasilisha mahakamani ombi la kukata rufaa.
KU hiyo ilitolewa Novemba 3, mwaka huu na Hakimu Mkazi Mkuu Mkoa wa Iringa Said Mkasiwa baada ya kujiridhisha kuwa ni kweli mjane huyo mwenye watoto wanne alikutwa na ndoo iliyokuwa na nyama hiyo yenye thamani ya Sh 900,000 kinyume na Sheria .
Akitoa hukumu hiyo kwa mjane huyo mkazi wa Zizi la Ng’ombe mjini Iringa, Hakimu Mkazi Mkoa wa Iringa, Mkasiwa alisema kosa hilo ni kinyume na kifungu cha 86 (1) (2) (c) cha sheria ya uhifadhi wa wanyamapori namba tano ya mwaka 2009 kama ilivyofanyiwa marekebisho na kifungu cha 59 (a) (b) cha mabadiliko ya sheria ya mwaka 2016.
Wakati akijitetea bila usaidizi wa wakili mjane huyo alikiri ni kweli alikutwa na ndoo yenye nyama hiyo ambayo alidai alikabidhiwa na mtu aliyemtambua kwa jina moja la Fute bila kujua ina nyama ya nini .
0 Comments