NA MWANDISHI WETU,ZANZIBAR
UMOJA wa Taasisi za Kusafirisha Mahujaji Zanzibar (UTAHIZA) umeziomba taasisi za Kifedha pamoja na Mabenk kurahisha upatikanaji wa Dola ili kutoa fursa kwa Mahujaji kukamilisha taratibu za Safari ya Hija bila ya changamoto yoyote mara baada ya mabadiliko ya Ibada ya Hija kutolewa Nchini Saudi Arabia kwa mwaka 2024.
Ibada ya Hijja ni muongoni mwa nguzo Tano za Uislam ambapo hutekelezwa nchini Saudi Arabia kila Mwaka kwa Muislam mwenye uwezo.
Akizungumza leo na Waandishi wa Habari kufuatia Mabadiliko mbalimbali yaliyotolewa na Wizara ya Hijja na Umrah Nchini Saudi Arabia juu ya Matakwa ya Ibada hiyo, Mwenyekiti wa Umoja wa Taasisi za Kusafirsha Mahujaji Zanzibar UTAHIZA, Sheikh Ali Ahlam Ali amesema, Mabadiliko hayo yanazitaka taasisi za Hijja kukamilisha taratibu za Safari mapema huku kikwazo kikiwa upatikanaji wa Dola ambao umekuwa haba Nchini.
"Nitumie fursa hii kuziomba taasisi za Kifedha hususani mabenki kuendelea kutupatia ushirikiano wao kwa kutuwezesha kupata fedha za Kigeni hasa dola za Kimarekani kila tunapozihitajika," amesema.
"Upatikanaji wa Dola umekuwa kikwazo kikwabwa katika kusafirisha Mahujaji ambapo tuiomba Serikali pamoja na taasisi za kifedha kurahisisha upatikanaji wa Dola ili kuondoa kikwazo hicho ukizingatia Wizara ya Hijja na Umra saudi Arabia imetoa utaratibu mpya wa Kukamilisha Ibada hiyo," Amesema.
Pia ameeleza kwamba, Mabadiliko yaliyotolewa na Wizara ya Hijja na Umrah Nchini saudi Arabia yanalengo la kuondoa changamoto za Ibada hiyo ambazo Mahujaji huksbiliana nazo.
"Niwaombe Waislamu wote pamoja na taasisi zote za kuafirisha Mahujaji kukamilisha Mapema utaratibu wa Safari ikiwemo usajili na malipo,"ameeleza.
"Tumekuiteni hapa kwa lengo la kutaka kusaidiana kuwahabarisha Umma juu ya mabadiliko haya ambapo muda wa kukamilisha usajili na mambo mengine yamebadilika kwa kiasi kikubwa,"amesema.
Mapema Sheikh Abdallah Talib Katibu Mtendaji wa Wakfu na Mali ya Amana Zanzibar amekanusha uwepo wa taarifa zinaonea kuwa Zanzibar inapokea tiketi za Bure kwenda kuhiji kutoka kwa Mfalme wa Saudi Arabia.
Idadi ya Waislamu wanaokwenda kutekeleza Ibada ya Hijja kwa mwaka Zanzibar ni zaidi ya 2500.
0 Comments