Ni katika madhimisho ya kilele cha siku ya mtoto wa kike duniani kwa mwaka 2023 ambapo maaadhimisho haya kwa mkoa wa iringa yamefanyika katika viwanja vya kichangani, Halmashauri ya Manispaa ya Iringa mjini.
Maadhimisho haya kila mwaka huadhimishwa Oktoba 11 ambapo Tanzania huungana na nchi wanachama wa Umoja wa Mataifa kuadhimisha siku hii ikiwa ni kuunga mkono kampeni dhidi ya ukatili kwa watoto hususani watoto wa kike.
Katika maadhimisho haya mgeni rasmi alikuwa ni Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mheshimiwa Halima Omary Dendego. Madhimisho haya kwa mwaka 2023 yamebeba kauli mbiu isemayo "Wekeza katika haki za wasichana, Uongozi wetu, Ustawi wetu".
Katika hotuba aliyoitoa katika maadhimisho hayo mkuu wa mkoa wa Iringa Mhe. Dendego amewaasa watoto kushtaki kwa wazazi, walezi au hata katika vyombo husika vya kushughulika na kupinga ukatili dhidi ya watoto pindi wanapofanyiwa ukatili katika jamii ili hatua za kisheria zichukuliwe kutokomeza ukatili dhidi ya watoto katika jamii.
Mkuu wa mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dendego anasema "katika mkoa wa iringa kupitia mpango wa TASAF tumefanikiwa kununua sare za shule (Uniform) kwa ajili ya watoto wanaotokea katika kaya maskini ili nao waweze kupata elimu kama watoto wengine."
Hata hivyo mkuu wa mkoa wa Iringa Mheshimiwa Dendego hajaridhishwa na kufurahishwa na idadi kubwa ya matukio ya ukatili dhidi ya watoto katika mkoa wa Iringa pia na ameahidi kuunga mkono Serikali na Taasisi mbali mbali zinazopambana na kupinga ukatili dhidi ya watoto.
0 Comments