Header Ads Widget

WAZIRI BASHUNGWA ATAKA WANANCHI KUTUNZA MIUNDO MBINU YA BARABARA


waziri wa Ujenzi Innocent Bashungwa akimshukuru Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi (CCM)mkoa wa Iringa Daud Yassin baada ya ziara yake mkoa wa Iringa 

..................................................................

WAZIRI wa Ujenzi Innocent Bashungwa amewataka wananchi kutunza miundo mbinu ya barabara zinazojengwa.


Waziri Bashungwa aliyasema hayo leo wakati wa hafla ya kusaini Mkataba wa Ujenzi wa mradi wa barabara ya lami yenye urefu wa kilomita 33.61 inayojengwa kutoka Ipogolo -Kilolo kwa kiasi cha Tsh bilioni 60.1


Alisema kuwa Serikali inaendelea kutekeleza Miradi ya barabara ndani ya mkoa wa Iringa na mikoa mingine ya Tanzania .


Pia alisema pamoja na mradi huo wa barabara ya Kilolo pia Rais Dr Samia ameiwezesha Wizara ya Ujenzi kuanza Ujenzi wa barabara ya Pawaga ,Sawala  Kwenda Mgololo ,Nyololo kwenda Kibao ,Pamoja na barabara ya Mchepuko ya Igumbilo -Tumaini Iringa.


Pia alisema Rais Dr Samia amemwagiza kutembelea eneo la Mlima Kitonga Ili kuangalia jinsi ya kutengeneza barabara ya Mchepuko katika Mlima Kitonga.


Akijibu maombi ya Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga kuhusu kero ya barabara waziri Bashungwa alisema Mbunge huyo amekuwa mfuatiliaji mkubwa wa changamoto za wananchi wa Kilolo .


Alisema Mbunge huyo ameendelea kutatua changamoto mbali mbali za wana Kilolo na kuwa barabara hiyo inakwenda kuwa Mkombozi mkubwa kwa wananchi wa Kilolo .


"Tunajivunia kuwa na wabunge wasikivu na wanaopigania wananchi wake kweli nitawashangaa sana wana Kilolo kama mtakwenda tofauti na Mbunge wenu mchapa kazi "

Waziri Bashungwa akiagana na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga 


Alisema kuwa kwa upande wake amekuja Kilolo Kwa niaba ya Rais Dr Samia hivyo hata maombi ya Mbunge Nyamoga ya kuomba kipande chenye urefu wa kilomita 17 kuwa cha vumbi ombi lake amelipokea na ataliweka kwenye vipaumbele vya Serikali .


Pia alisema kuhusu changamoto ya Mlima Msonza ambako wananchi wamekuwa wakipata kero Kubwa Wizara itahakikisha changamoto ya eneo Hilo inatatuliwa kwa kujenga kilomita Moja ya lami .


"Lakini Mbunge Nyamoga ameomba barabara ya Mchepuko Mlima Kitonga hili pia tunakichukua pamoja na lile la barabara ya Ilula "alisema waziri Bashungwa 



Kwa upande wake mkuu wa mkoa wa Iringa Halima Dendego alisema  toka Serikali ya awamu ya sita imeingia madarakani imepokea fedha nyingi zaidi za barabara ndani ya mkoa huo .


Alisema toka Rais Dr Samia Suluhu Hassan ameingia madarakani fedha za Miradi ya barabara na Miradi mingine zimeendelea kufika kwa wakati ndani ya mkoa huo .


Alisema mbali ya Miradi ya barabara pia mkoa umeendelea kupokea fedha za Miradi ya Maji na tayari Miradi mitano imekwisha sainiwa ndani ya wiki hii .


Hata hivyo alisema kuwa kuhusu umeme mkoa umeendelea kupokea fedha za Miradi ya umeme na mategemeo ya mkoa kuona vijiji na vitongoji vyote vinawashwa umeme .


Alisema kuwa kiasi cha Tsh Bilioni 18.9 zimekwisha pokelewa kwa ajili ya Sekta ya elimu kwa ajili ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa ndani ya mkoa wa Iringa.


Aidha alisema kuwa katika Sekta ya kilimo mkoa wa Iringa umeendelea kufanya vizuri na kushuhudia jitihada za Serikali za kumpunguzia mzigo mkulima kwa kuweka ruzuku ya mbolea na hivyo kuongeza uzalishaji wa mazao kwa wakulima .


Pia alisema mkoa huo una hekta 210000 za Miradi ya umwagiliaji  ikiwa ni pamoja na mkoa kuendelea kuimarisha Vyama vya ushirika Ili kuondoa kero ya wakulima kuendelea kuibiwa na walanguzi wa mazao.


Kuhusu Sekta ya Ujenzi mkuu huyo wa mkoa alisema kuwa mkoa umepokea fedha za upanuzi wa Uwanja wa Ndege wa Iringa.


Huku katika miundo mbinu ya barabara Wilaya ya Kilolo ilikuwa ni ya mwisho kwa barabara ila Sasa inakwenda kupata barabara Bora zaidi yenye urefu wa kilomita 33.61 kuliko Wilaya zote ndani ya mkoa wa Iringa .


Awali Mbunge wa  viti maalum mkoa wa Iringa Ritta Kabati na Mbunge wa Jimbo la Kilolo Justin Nyamoga pamoja na kupongeza Serikali kwa Ujenzi wa barabara hiyo Bado waliomba kuongezewa barabara zaidi kuelekea maeneo ya vijijini zaidi .


Mbali ya hafla ya utilianaji sahini Ujenzi wa barabara ya Iringa -Kilolo Waziri Bashungwa alitembelea barabara ya mchepuko ya Tumaini Igumbilo mjini Iringa inayotarajiwa kupunguza msongamano wa magari hususani maroli na magari mengine makubwa yanayopita katikati ya mji wa Iringa.


Mbunge wa Jimbo la Iringa Dk Jesca Msambatavangu amezungumzia umuhimu wa barabara za mjini Iringa kuimarishwa akisema zina mchango mkubwa kiuchumi na ukuaji wa sekta ya utalii.

Dk Msambatavangu alisema magari hayo makubwa yamekuwa kero kwa watumiaji wengine wa barabara za mjini wakiwemo watalii jambo linalopunguza kasi ya maendeleo mengine.

MNEC na Mwenyekiti wa kamati ya usalama Barabarani mkoa wa Iringa Salim Abri Asas akishukuru 

Huku Mwenyekiti wa Kamati ya Usalama Barabarani Mkoa wa Iringa Salim Asas alisema kukamilika kwa barabara hiyo ya mchepuko kutapunguza msongamano, muda wa kusafiri, ajali na kuongeza usalama wa watumiaji wa barabara za katikati ya mji.

“Kwa hiyo barabara hiyo ya mchepuko ina jukumu muhimu katika kuboresha mfumo wa usafirishaji na kuongeza ubora wa maisha kwa wakazi na wageni wa Iringa mjini,” alisema Asas ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa.


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI