Na Fadhili Abdallah, Kigoma
WANANCHI 1500 kutoka maeneo mvalumbali ya mkoa Kigoma wanatarajia kunufaika na huduma za matibabu kutoka kwa madaktari bingwa 11 kutoka China.
Mbunge wa jimbo la Kigoma kaskazini wilaya ya Kigoma mkoani Kigoma, Asa Makanika alisema hayo katika uzinduzi wa utoaji wa huduma hizo uliofanywa na Balozi wa China nchini, Chen Mingjian.
Makanika alisema kuwa huduma mbalimbali zitatolewa ikiwemo huduma za upasuaji,dawa na vifaa tiba ambavyo vitatolewa bila malipo katika vituo vya afya vya Bitale na Simbo kuanzia Oktoba 15 hadi 20 mwaka huu.
Makanika alisema kuwa pamoja na kazi kubwa inayofanywa na serikali katika kuimarisha na kuboresha huduma za afya mkoani humo lakini bado huduma za madaktari mabingwa zimekuwa changamoto kubwa kutokana na kutowepo kwa idadi ya kutosha ya Madaktari bingwa mkoani humo.
Mbunge huyo alisema kuwa kutokana na hali hiyo alifanya jitihada kubwa kufanikisha ujio wa madaktari hao katika jimbo hilo.
Akizungumza katika uzinduzi huo Balozi wa China nchini Tanzania,Chen Mingjian
alisema kuwa kambi hizo za madaktari bingwa ni sehemu ya mahusiano yaliyoanzishwa na waasisi wa mataifa ya China na Tanzania ambayo yalianza mwaka 1964 ambapo mwaka 1968 China ilianza kutuma madaktari Nchini Tanzania na tayari wagonjwa milioni 20 wamepatiwa matibabu na madaktari hao kwa safari 26 walizofanya Tanzania bara na safari 32 kwa Zanzibar.
Balozi Chen alisema kuwa hadi sasa Watanzania milioni 20 wamenufaika na huduma za matibabu ya kibingwa kutoka kwa madaktari Bingwa kutoka China ambao wamekuwa wakiendesha kambi mbalimbali za matibabu nchini.
Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma, Dk. Jesca Leba ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye kwenye uzinduzi huo alisema kuwa mkoa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa asilimia 60 wa watoa huduma za afya na vifaa vya matibabu na upatikanaji wa huduma ya madaktari bingwa ni changamoto kubwa mkoani humo.
Mganga Mkuu wa mkoa Kigoma,Dk.Jesca Leba ambaye alimwakilisha Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye kwenye uzinduzi huo alisema kuwa mkoa Kigoma unakabiliwa na upungufu wa asilimia 60 wa watoa huduma za afya na vifaa vya matibabu na upatikanaji wa huduma ya madaktari bingwa ni changamoto kubwa mkoani humo.
0 Comments