NA CHAUSIKU SAID-MATUKIO DAIMAAPP MWANZA .
Mkuu wa Operesheni za jeshi la polisi Nchini Mihayo Msikhela amesema kuwa jeshi la polisi liko tayari kuendelea kushirikiana na wadau wa Uvuvi Nchini dhidi ya uhalifu unafanyika katika ziwa Victoria ndani na nje ya Nchi.
Kauli hiyo ameitoa leo jijini Mwanza wakati wa utoaji wa tathimini ya kikao kilichofanyika Mkoani Geita dhidi ya uhalifu ziwa Victoria na kupanga mikakati ya kuzuia na kupambana na uhalifu huo ndani ya ziwa.
Msikhela amesema kuwa mwaka 2019- 2021 kuliibuka uharifu mkubwa ndani ya ziwa Victoria unyang'anyi wa kutumia silaha, kutumia nguvu, wizi wa nyavu za kuvulia samaki, injini za boti, boti, mafuta pamoja na uporaji wa samaki na kusababisha malalamiko makubwa.
"Sehemu kubwa ya uchumi uliokuwa unazunguka ziwa Victoria kukawa na sintofahamu Kwa ndugu zetu wavuvi wanaoshinda siku nzima ndani ya ziwa Victoria" Alisema Msikhela.
Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana Amina Makilagi akizungumza Kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa Mwanza Amos Makalla ameeleza kuwa wamezamilia kutekeleza mpango wa maendeleo Kwa miaka mitano itakayosaidia sekta ya uvuvi na kuifanya Mwanza kuwa na uchumi wa blue.
"Tasnia hii ya uvuvi ni muhimu katika utoaji ajira na kuongea kipato Kwa mtu moja moja na ni miongoni mwa sekta muhimu zinazochangia na kuondoa umasikini na kukuza uchumi katika Mkoa wa Mwanza na Taifa Kwa ujumla" Alisema Makilagi.
Makila amesema kuwa Kwa mjibu wa takwimu zilizopo sekta ya uvuvi inachangia Pato la Mkoa Kwa asilimia 7 na shughuli za uvuvi ni kubwa ukiringanisha na sekta zingine.
Ameeleza kuwa Shughuli za uvuvi zimeendelea kutoa mchango mkubwa Kwa uchumi na maendeleo ya wananchi Kwa Mkoa wa Mwanza Kwa kuwapatia lishe bora, ajira na kipato Kwa ujumla
"Kwa mujibu wa takwimu za sensa tulizozipata hivi juzi zinaeleza sekta za uvuvi ni miongoni mwa sekta ambazo zinamuwezesha mwananchi wa chini ambaye anaweza kuwa na mtaji mdogo na akaweza kujinufaisha na akaweza kupata naendeleo sio kwamba imeishia Kwa watu wakubwa imeweza kupenya Hadi Kwa watu wadogo.
Kwa upande wake M/mwenyekiti wa kamati ya ushauri uvuvi endelevu ziwa Victoria Hasani Mhenga ameeleza kuwa jeshi la polisi limesaidia kuondoa uhalifu ndani ya Ziwa Victoria wa wizi wa kunyang'anyana mashine umeweza kutoweka
Kwa upande mwingine ameliomba jeshi la polisi kuwasidia uhalifu kuthibiti wizi wa wao Kwa wao ulioibuka wa kunyang'anyana mali, wivu wa Mali, wizi wa nyavu na taa za kuvulia samaki.
0 Comments