Header Ads Widget

NYUMBA 106 ZAEZULIWA NA UPEPO KAGERA MMOJA ADAIWA KUFA

 



Mtu mmoja anadaiwa kupoteza maisha na nyumba 106 kuezuliwa na upepo katika manispaa ya Bukoba mkoani Kagera, kufuatia mvua kubwa iliyonyesha ikiwa imeambatana na upepo mkali alfajiri ya leo.


Akizungumzia tukio hilo Mkuu wa Wilaya ya Bukoba Erasto Sima, amesema kuwa polisi wanaendelea na uchunguzi kuhusiana na kifo hicho maana inaonekana ni mwili uliosombwa na maji.


"Serikali tunaendelea kuchukua hatua za haraka kutafuta makazi kwa ajili ya wananchi ambao nyumba zao zimeezuliwa na kusababisha wakose pa kulala" amesema Sima.


Baadhi ya wakazi wa  manispaa ya Bukoba ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo akiwemo Eradius Gabriel mkazi wa Majengo Mapya, wameiomba serikali na wadau wengine kuwasaidia kupata mahala pa kuishi, chakula  na kurejeshewa miundombinu ya umeme.



"Kwa sasa hatuna chakula na hatuna pa kulala, imeanza mvua kidogo kidogo baadae ukatoka upepo mkali na kama mnavyoona jengo letu limeathirika na majirani pia, amesema Gabriel


Askofu Msaidizi Jimbo Catholic la Bukoba Methodius Kilaini amesema kuwa kanisa la Parokia ya Rwamishenye limeezuliwa na kuwaomba wananchi kushirikiana kutoa msaada kwa walioathirika ili wapate chakula na malazi.


"Kama kanisa tumepata madhara makubwa kwa sababu Rwamishenye ni Parokia mpya, hivyo sote na waumini wengine tuwe kitu kimoja katika kusaidia watu hawa kwa sababu sasa hivi hawana mahala pa kusalia na mapadre hawana pa kulala". amesema Askofu Kilaini.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI