Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WAKALA wa ufundi na umeme (TEMESA) umesema kuwa mabadiliko makubwa ya kiutendaji yanayofanywa na wakala huo yanalenga kuondoa malalamiko ya wateja wanaoleta magari yao kwenye karakana za wakala huo.
Mtendaji Mkuu wa TEMESA,Razalo Kilahala alisema hayo katika kikao cha wadau kutoka Idara za serikli na taasisi zaeke wanaopeleka magari yao kufanyiwa matengenezo kwenye karakana za wakala huo ambapo amesema kuwa mabadiliko hayo wamezingatia maoni yote kuhusu utendaji wao.
Kilahala alisema kuwa moja ya changamoto kubwa ya malalamiko ya wateja ni gari kukaa muda mrefu, gharama kubwa za vifaa na matengenezo, gari kuwekewa vifaa vilivyo chini ya kiwango na kwamba mambo yote hayo yamefanyiwa marekebisho kwa kuingia mkataba na wakandarasi watakaosambamba vifaa kwenye karakana zao vifaa vitakavyozingatia ubora na bei ya soko.
Akifungua mkutano huo Mkuu wa mkoa Kigoma,Thobias Andengenye alisema kuwa changamoto kubwa ya utendaji wa TEMESA ni pamoja na idara na taasisi za serikali kushindwa kulipa madeni yao kwa kufanya matengenezo ya gari zao kwa mkopo hivyo wakala huo kutokuwa na uwezo wa kununua vipuri kwa wakati.
Alisema kuwa ili kuondoa changamoto hiyo ametaka kila mdau kutimiza wajibu wake kwa TEMESA kutengeneza magari kwa wakati na kuzingatia ubora hasa wakati huu ambapo serikali imenunua vifaa vua kisasa kwa karakana zote za TEMESA nchini lakini pia kuwataka wadau wote wanaopeleka magari yao kwenye wakala huo kulipa madeni yao wanapoletewa bili za matengenezo.
0 Comments