Na mwandishi wetu , Mtwara
Taasisi isiyokuwa ya kiserikali ya ADEA iliyopo mkoani Mtwara, inatarajia kufanya Tamasha la ngoma za asili la MAKUYA, litakalokutanisha makabila matatu ya Makonde, Makua na Yao, kwa lengo la kutangaza mila na desturi za makabila hayo ikiwemo tamaduni na aina za vyakula walivyokuwa wanakula.
Akizungumza wakati wa maandalizi ha tamasha hilo Mkurugenzi lililodhaminiwa na Ubalozi wa Tanzania, Uswiss na Norway ambao ndio wafadhili wakuuSaid Chilumba alisema kuwa Mnamo , Oktoba 21, 2023 katika viunga vya mji wa Mtwara vikundi saba vyenye jumla ya watu 100 vitashiriki katika tamasha hilo kutoka vijiji mbalimbali ndani ya Mkoa wa Mtwara vitatumbuiza aina mbalimbali za Ngoma za asili.
"Makuya ni tamasha hujumuisha pia a wachongaji wa vinyago vya kimakonde, mafundi chuma, wasusi wa vikapu, wachorajina mafundi cherehani ili kusisimua ubunifu wao"
"Tamasha hili linaenda kutimiza malengo endelevu ya kuwaleta wasanii kutoka vijijini na kuwaleta pamoja kutoka katika mkabila matatu Wamakonde, wamakuwa na wayao ambapo watacheza ngoma za asili, maonyesho ya michezo ya jadi, maonyesho vit vya asili vya wanajamii? amesema Chilumba
Nae Mwenyekiti wa bodi ya shirika la ADEA Tiago Mtanda amesema kuwa taasha hilo linaenda kuongeza idadi ya watalii na kukuza utaliii mkoani hapana sambamba na kuongezeka fursa za kibiashara ikiwemo kwenye nyumba za kulala wageni"
0 Comments