Na Elizabeth Ntambala ,Rukwa
JESHI la Polisi Mkoani Rukwa linawashikilia watu watatu kwa tuhuma za mauaji ya Baraka Markusi Nyangala (30) mfanyabiashara mkazi wa mtaa wa Kasisiwe katika Manispaa ya Sumbawanga.
Akizungumza na wanahabari Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Rukwa, ACP, Shadrack Masija alisema kuwa Watuhumiwa hao walimuuwa kwa kumpiga na Rungu kichwani kisha kuchimba shimo na kumfukia akiwa hai.
ACP Masija akizungumzia tukio Hilo alisema kuwa Watuhumiwa hao wa mauaji walifanya tukio Hilo Septemba 28 mwaka huu baada ya kumpigia simu marehemu kumjulisha kuwa kuna maharage wanauza.
Kamanda Masija alidai kuwa baada ya kukubaliana alikwenda kijiji Cha Katazi wilaya ya Kalambo kwa ajili ya kununua maharage wakiwa wote wanne ndipo walipofika porini walitimiza Nia Yao ya kumpiga Rungu kichwani.
Alisema kuwa Marehemu akiwa na Watuhumiwa hao walifanikiwa kumnyang anya fedha Tsh 1,840,000 pamoja na pikipiki na baada ya kitendo hicho walichimba shimo na kumfukia akiwa hai.
Aliongeza kuwa Taarifa ya kupotea kwa Baraka Nyangala zilifika polisi na ndipo Uchunguzi ulifanyika kwa kuwatumia intelejensia na wataalamu wa cyber crime na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa ambao wakaongoza mpaka eneo walilomfukia marehemu.
Alisema kuwa lengo la tukio Hilo ni unyang'anyi wa Mali kutoka kwa marehemu na kutoa wito kwa jamii kuacha tamaa za kupata utajiri au Mali za haraka haraka pasipo kufanya kazi halali.
Aliwataja Watuhumiwa hao kuwa ni Frank Simsokwe (33) , Edfonsi Simsokwe (28) na Niikas Lunguya (38) ambao baada ya kuhojiwa walikiri na kwenda kuonyesha eneo walilomfukia.
0 Comments