Header Ads Widget

RAIS SAMIA - HAKUNA SAUTI ILIYOPUUZWA KUHUSU BANDARI YA DAR ES SALAAM

 




Na Hamida Ramadhani, Matukio daima APP Dodoma


RAIS wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan amesema hakuna sauti iliyopuuzwa katika maoni yaliyotolewa kuhusu Mkataba ya Uwekezaji Bandari ya Dar es Salaam ambapo mikataba iliyosainiwa imezingatia sheria za nchi na maoni kutoka makundi mbalimbali.


Akizungumza baada ya kushuhudia utiaji saini wa mikabata mitatu ya ukodishaji na uendeshaji wa Bandari ya Dar es Salaam, Ikulu ya Chamwino mkoani Dodoma, Rais Dk. Samia amesema  bandari hiyo ni kuinganishi muhimu cha biashara baina ya Tanzania na mataifa yanayoizunguka.


Amesema kupitia makubaliano hayo shughuli za biashara zinakwenda kukua ndani ya nchi na hata nchi jirani


Aidha amesema mikataba yote iliyosainiwa imezingatia maoni na maslahi mapana ya nchi kwani hakuna mtanazania au mfanyakazi yoyote wa bandari atakaepoteza kazi badala yaka itabadilika mifumo ili kuendana na viwango vya Kiteknolojia. 






Kwa upande wake, Makamu wa Rais Dkt. Philip Mpango, amesema takwimu kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) zinaonyesha kuwa asilimia 26 ya Watanzania wanaishi chini ya kiwango cha umasikini.



Amesema nchi ya Tanzania imejaliwa rasilimali ambapo umasikini uliopo haiendani na hali halisi ya nchi ilivyo hivyo ni champion kuendelea kukuzalia rasilimali tulizonazo hali itakayopelekea kuwakomboa wa Tanzania kutoka kwenye umasikini huo. 


" Lakini pia ukweli ni kwamba dunia ya sasa imejaa ushindani mkubwa hivyo kama bandari isipokuwa na tija basi biashara itakwenda kwingine, "amesema Dkt Mpango. 


Awali Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Usimamizi wa Bandari Tanzania TPA Plasduce Mbossa amesema Mikataba hiyo imezingatia vitu vingi kwa Maslahi ya nchini.


Pia amesema mkataba huo uta kuwa na ukomo wa muda wa Miaka 30 na siyo miaka 100 kama baadhi ya watu wanavyosema na utapimwa kila baada ya miaka 5.


" Mwekezaji atalipa kodi zote kwa kufuata sheria za Tanzania ambapo sheria hizo za Tanzania ndizo zitakazotumika kwenye mikataba hiyo na serikali ya Tanzania itakuwa haki kuuondoa mkataba huo pale itakapobidi, " Amesema Mkurugenzi huyo. 





Mwisho

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI