Na Gift Mongi, Matukio DAIMA APP, MOSHI
Kutokana na majukumu ya kiutendaji na kibunge yanayomkabili mbunge wa jimbo la Moshi Vijijini Prof Patrick Ndakidemi yamempelekea kushindwa kuhudhuria Katika mahafali ya 19 ya shule ya sekondari Sungu ambapo alilazimika kuwakilishwa na
diwani wa Kata ya Kibosho Mashariki Christopher Ndakidemi.
Mkuu wa shule akizungumza kwa niaba ya uongozi wa shule Mwl. James Warburg, alimshukuru mgeni rasmi pamoja na wageni wengine waliohuhudhuria katika mahafali hayo kwani huo ni muendelezo katika kukuza sekta ya elimu
Katika hafla hiyo Prof Ndakidemi alichangia kiasi cha shilingi milioni 4.5 kwa ajili ya ujenzi wa jiko jipya kwani ndiyo changamoto kubwa inayowakabili.
Wageni mbali mbali waliohudhuria hafla hiyo wakiwemo viongozi wa Chama Cha Mapinduzi Kata, bodi ya shule, waalimu wa shule za jirani pamoja na Afisa Mtendaji Kata na viongozi wengine wa Serikali ya Kijiji cha Sungu.
Miongoni mwa wazazi wenye wanafunzi shuleni hapo Christopher Lyamuya alisema kila mzazi anao wajibu katika kukuza sekta ya elimu badala ya kuiachia serikali pekee.
'Niseme kila moja wetu anao wajibu katika kuchangia sekta ya elimu na sio Kwa kuiachia sekta binafsi ama serikali pekee Kwa namna hiyo hatutasonga mbele'anasema
Aliongeza kuwa wazazi na walezi wanao wajibu wa kurudisha fadhila kwa shule ambazo watoto wao wamesoma kwani hiyo inaleta hamasa na kupanua wigo wa elimu kwa nyanja mbalimbali
Neema Nkya moja wa wanafunzi shuleni hapo alisema mwitikio wa wadau mbalimbali kujitokeza katika nyanja ya elimu inaonesha ni jinsi gani watu walivyo na mwamko katika elimu.
Mwisho.
0 Comments