Header Ads Widget

AHUKUMIWA MIAKA 180 KWA MAKOSA (6) YA UBAKAJI NA ULAWITI MKOANI NJOMBE.

 



Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Mahakama ya wilaya ya Njombe imemuhukumu Juma Msemwa kijana wa miaka 27 na mkazi wa Njombe, kutumikia  kifungo cha miaka 180  jela kwa Makosa 6 ya ulawiti na ubakaji. 


Katika mahakama ya wilaya ya Njombe,hukumu imesomwa kwa zaidi ya dakika 45, na baadae mahakama ikahitimisha kwa kumtia hatiani Juma Msemwa kutumikia kifungo cha miaka 180 kwa makosa sita na kila kosa miaka 30.


Akisoma hukumu hiyo ya shauri namba 53 la mwaka 2023, Hakimu mkazi wa wilaya ya Njombe Matilda Kayombo, amesema mshtakiwa Joseph amekutwa na hatia katika makosa sita, matatu yakiwa ni ubakaji na matatu ya ulawiti anayodaiwa kuyafanya siku ya tarehe 16 hadi 23 mwezi mei mwaka 2023 katika mtaa wa kihesa kilimani, Mkoani Njombe.


Matilda ameendelea kusema mahakama imemtia hatiani baada ya kusikiliza ushahidi uliotolewa na mashahidi saba, wakiwemo waathirika wa matukio, Taarifa ya uchunguzi wa Daktari, uongozi wa serikali ya mtaa pamoja na Polisi.


Kijana Juma Msemwa anadaiwa kutenda makosa hayo kwa nyakati tofauti, baada ya kuwahadaa wanawake watatu na kisha kuwafungia katika nyumba aliyokuwa anaishi katika mtaa wa kihesa, na kisha kuwalawiti na kuwabaka kwa zamu usiku na mchana, zoezi lililoenda sambamba na kuwaingiza magunzi ya mahindi na matango katika sehemu za siri.


Taarifa zilizosaidia kukamatwa kwake zinaelezwa na mahakama kuwa zilitolewa na mmoja kati ya wanawake aliokuwa amewateka, ambae alifanikiwa kutoroka na kupiga ndulu kwa majirani ambao walivamia nyumbani kwa Juma na kukuta wanawake wengine wawili wakiwa ndani, vile vile kulikutwa mfuko ukiwa na dawa za kienyeji, huku mahakama ikieleza kuwa sehemu ya ushahidi uliotolewa ulibainisha kuwa mtuhumiwa baada ya kuhojiwa alikiri kwamba alifanya matukio hayo akiwa anatekeleza maagizo ya mganga aliyemtaka abake wanawake na watoto.


Waendesha mashtaka wakiongozwa na Magdalena Whelo na Elicy  James waliiomba mahakama kutoa hukumu kali kwa mtuhumiwa ili iwe funzo kwa jamii yote ikizingatiwa kwamba matukio ya ubakaji na ulawiti yamekuwa yakiongezeka mkoani  Njombe.


Baada ya mahakama kujiridhisha na ushahidi uliotolewa,mahakama imemhukumu Juma Msemwa kutumikia miaka 30 jela kwa kila kosa, katika makosa yote sita aliyokutwa nayo, ambayo ni kinyume na kifungu cha sheria namba 130 kifungu kidogo cha kwanza na cha pili (e) sambamba na kifungu kidogo cha kwanza cha sheria ya adhabu kifungu namba 16 kama ilivyofanyiwa marejeo mwaka 2022.


Hukumu hiyo inakwenda sambamba na kulipa fidia ya fedha halali za kitanzania kiasi cha shilingi milioni moja, kwa kila muathirika wa makosa aliyoyafanya.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI