Header Ads Widget

NMB YAKABIDHI VIFAA VYA AFYA NA ELIMU KILWA

 

Na Hadija omary,LINDI 

 BENK  ya NMB Kanda ya kusini imekabidhi vifaa mbali mbali vya afya na elimu vyenye thamani ya Zaidi ya milioni 25 katika halmashauri ya kilwa mkoani lindi kwa lengo la kurejesha kwa jamii faida waliyoipata

 

 

Akizungumza wakati wa kukabidhi vifaa hivyo jana Meneja wa NMB kanda ya kusini Faraja Ng'ingo alisema vifaa hivyo vilivyokabidhiwa Madawaiti na vifaa vya kuezekea kwa shule ya msingi songomnara, miguruwe, mnazi mmoja pamoja na vitanda, Magodoro na mashuka kwa kituo cha Afya somanga

 

Amesema vifaa walivyokabidhi ni moja ya ushirikiano wao katika maendeleo ya jamii na wao kama benki inayoongoza wanao wajibu wa kuhakikisha jamii inayowazunguka inafaidika kutokana na faida wanayoipata

 

 

Meneja Ng'ingo alibainisha kuwa Changamoto za sekta ya elimu na Afya Tanzania kwa Benki ya NMB ni jambo la kipaumbele na hiyo ni kutokana na ukweli kwamba Elimu ndio ufunguo wa maendeleo kwa taifa lolote hapa ulimwenguni 


" tunatambua juhudi za serikali ya awamu ya sita  chini ya mheshimiwa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan za kusimamia upatikanaji wa Elimu bora kwa nguvu zote kwa kuboresha mazingira ya utoaji wa huduma hizi mjini na vijijini hatuna budi kuipongeza kwa hilo".

 

Akipokea vifaa hivyo katibu tawala Wilaya ya kilwa yusuph Issa kwa niaba ya Mkuu wa Wilaya hiyo aliwashukuru NMB kwa msaada walioutoa huku akieleza kuwa kitendo hicho kimeonyesha ni kwa namna gani benk hiyo inaunga mkono jitihada za serikali katika kuwahudumia wananchi wake katika sekta za afya na elimu

 

“kama inavyoeleza hiki tunachokipata kuwa ni kile tunachokiweka kinarudi, licha ya kupata faida ya kuhifadhiwa fedha zetu na zikawa salama lakini pia faida inayotokana na hilo tunaona ni namna gani inarudi kwa jamii tunawashukuru sana”

 

 




Mwalimu Mkuu wa Shule Mmnazi mmoja Ahamed Ally alisema kuwa kwa msaada walioupata umeweza kuwasaidia kufanya ukarabati wa Madarasa manne kati ya madarasa kumi yaliyopo katika shule hiyo yanayohitaji kufanyiwa ukarabati

 

Nae Mganga Mfawidhi wa kituo cha Afya Somanga Leonard Lucas  ameeleza kuwa vitanda na magodoro walivyovipata vitawasaidia kwa kiasi kikubwa akinamama wajawazito wanaokwenda kituoni hapo kupata huduma kwani kabla ya uwepo wa vitanda hivyo akina mama hao walikuwa wakilazimika kulala Zaidi ya mmoja wakusubiri kujifungua ama hata baada ya kujifungua

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI