Wajumbe wa Bodi ya Wakurugenzi wamekutana na wafanyabiashara wa mbolea wa Mikoa ya Mbeya, Songwe, Rukwa na Katavi kujadili masuala mbalimbali yanayohusiana na mfumo wa usambazaji wa mbolea za ruzuku.
Akizungumza wakati wa kikao hicho, Mwenyekiti Dkt. Diallo amesema ni muhimu sana kusikiliza na kutatua changaomoto za mawakala ili kuwezesha wakulima kununua mbolea kwa wakati.
Akiongoza majadiliano hayo Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi, Dkt. Anthony Diallo ameeleza nia ya kufanya kikao kazi hicho kuwa ni kusikiliza kero mbalimbali zitokanazo na mfumo wa ruzuku, kuzitolea majibu na kupata maoni ya mawakala yatakayoongeza ufanisi yatachukuliwa na kufanyiwa kazi na wataalamu wa Mfumo waliokuwa sehemu ya kikao hicho.
Akizungumza baada ya kikao hicho, wakala wa mbolea, Raban James amesema, kikao hicho kimejibu maswali mengi ya mawakala ikiwa ni pamoja na kutatua baadhi ya changamoto za kimfumo na kueleza kazi kubwa imefanyika katika kuboresha mfumo huo.
"Kwakikao hiki sisi mawakala tutaweza kupeleka mbolea maeneo ya vijijini kwani Mamlaka ipo tayari kupokea mapendekezo ya bei kwa kuzingatia umbali halisi na ugumu wa kufikika kwa maeneo husika" Laban alimaliza.
0 Comments