Header Ads Widget

MEYA AKABIDHI JEZI KWA TIMU YA WASICHANA YA NALIQEENS YA KITUO CHA TARI NAELINDELE

 


Na Mwandishi wetu, Mtwara


Meya  wa Manispaa ya Mtwara Mikindani Shadida Ndile ametoa jezi kwa timu ya mpira ya NaliQeens ili kuwahamasisha kuendelea kupenda michezo na kuwatia moyo.


“Leo nimekuja kuwatembelea Naliqeens ambapo nimewakabidhi jezi na mpira ili kuimarisha michezo kwa watoto wa kike ambapo wananafaisi kubwa ya kucheza na wakaonekana na kutimiza malengo yao ya kucheza soka” alisema Ndile 


Nae Yusra Matui mchezaji wa Naliqeens  amesema kuwa wamepata jezi meya, mashabiki na Tari kituo cha nalindele waendelee kuwapa moyo.


"Tumepata jezi na kuisapoti timu yetu tunaamini kuwa mchango wake ni mkubwa kwetu na ametuhamasisha sisi kama watoto wakike” 


Nae Janeth Petro kepten wa timu hiyo alisema kuwa wamekuwa wakitumia muda mwingi kujiandaa ambapo wanatarajia ushindi kwa timu yoyote watakayo cheza nayo.


Mratibu wa Uhaurishaji wa Teknolojia na Mahusiano kituo cha Tari Naliendele Rashid Kidunda alisema kuwa jezi hizo zinaenda kuwapa moli na nafasi ya kucheza vizuri na kutangaza kituo cha utafiti wa kilimo Tanzania. 


“Leo tumekumbukwa kupitia timu yetu ya mpira wa miguu kwa wasichana ambapo wamepata jezi ambazo zitawasaidia katika michezo mbalimbali ambapo kupitia michezo ni fursa kwetu tunaamini kuwa tunaweza kutangaza teknolojia zetu kupitia michezo hiyo hivyo tunahaurisha teknolojia kwa namna mbalimbali ambapo mchango wake utakuwa na msaada mkubwa kwa taasisi yetu” alisema Kidunda 


kwa upande wake Mratibu wa Ubunifu na Utafiti wa kituo cha TARI Naliendele Michezo ni sehemu muhimu ambapo kupitia michezo tumekuwa tukionyesha kazi zetu za kiutafiti.


“Tunazalisha teknolojia nyingi lakini tunabaki nazo kwenye makaratasi kupitia michezo tunaenda kuzitoa kwa wakulima kupitia michezo ni sehemu moja wapo ambao inaweza kurudisha majibu kwao kuhusu mazao mbalimbali ” alisema Dr Nene




Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI