ZAIDI ya mipira 25 yenye thamani ya Milioni 3 imekabidhiwa na chama cha RUNALI Kwa mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo Kwa ajili ya kukuza vipaji vya mpira wa miguu wilayani humo.
Akizungumza wakati wa kukabidhi mipira hiyo makamu mwenyekiti wa RUNALI Ahamadi Ngabuma alisema kuwa wametoa mipira 25 kwa lengo la kurudisha faida kwa jamii ambao wamekuwa wadau wakubwa wa kilimo na kutumia chama hicho katika kunufaika na kilimo Chao.
Kwa upande wake mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo aliwapongeza RUNALI Kwa kurudisha kwa jamii faida wanayoipata na kuahidi kuwa mipira hiyo 25 ataigawa Kwa timu zote zenye uhitaji akiwa kwenye ziara zake za kikazi huko vijijini.
0 Comments