Header Ads Widget

MBARAWA KUTOKURIDHISHWA NA UTENDAJI WA TRC KIGOMA

 


Na Editha Karlo Matukio Daima, Kigoma

Waziri wa  Ujenzi Pro. Makame Mbarawa ameonyesha kutoridhishwa utendaji wa kazi wa watumishi wa  Shirika la Reli nchini TRC  ya Kigoma kwa kushindwa kusimamia shirika na kutoa huduma bora kwa wateja wao.


Profesa Mbarawa ametoa kauli hiyo mara baada ya kutembelea ofisi ya reli Kigoma na Kukagua mabehewa ya kubeba mizigo ambapo amesema utendaji kazi mzuri wa reli unategemea ufanisi mzuri wa watumishi walio tayari kufanya kazi.


‘Ni vyema wale ambao wanaona hawawezi  kufanya kazi watupishe kuliko  kuendelea kuharibu taswira ya shirika kwani Serikali imeendelea kuweka pesa ili kuhakikisha wananchi wanapata huduma bora zaidi na kwa wakati”Alisema Mbarawa


Aidha Pro. Mbarawa ameagiza uongozi wa reli kupunguza muda wa treni kuleta mizigo kwani wanatumia muda mrefu wa takribani wiki mbili kutoka Tanga hadi kufika Kigoma na kuchelewesha huduma kwa wananchi.


’Unakuta treni ya Simenti inatoka Tanga kuja Kigoma njiani inatumia wiki mbali na bado ikifika inachelewa kupakua hali hii haiwezi kuleta manufaa kwa Shirika na Serikali kwa ujumla na hivyo kaeni muone namna ya kupunguza muda angalau hata siku tano hivi anasema Mbarawa’


Naye Kaimu Mkurugenzi  Mkuu wa Shirika la Reli Bw. Senzige Kisenge amesema licha changamoto zinazowakabili hususani njia ya reli kutoka Kigoma hadi Tabora kuwa mbovu na treni kutembea polepole njiani lakini wataendelea kuboresha ili kuhakikisha wanakidhi mahitaji kwa wateja.


Kwa upande wao baadhi ya wafanyabiashara na wananchi wa Mkoa wa Kigoma wamesema ucheleweshaji wa mabehewa kupakua na kupakia mizigo imekuwa ikisababisha kukosa huduma zenye ubora na wengi wao kuingia gharama kubwa za uendeshaji wa biashara zao.


“Tunapenda kutumia usafiri wa treni kusafirisha mizigo yetu ya biashara tatizo kuna ucheleweshaji sana kupakua na kupakia mizigo kwenye mabehewa hali inayofanya kuonekana shirika la reli linatoa huduma ambazo hazina ubora”alisema mfanyabiashara mmoja.

Waziri wa ujenzi Pro.Makame Mbarawa akichukua maelezo toka kwa Kaimu mkurugenzi mkuu wa shirika la reli Senzigr Kisenga(mwenye shati nyeupe)baada ya kutembelea mabehewa ya kubeba mizigo


Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI