NA ARODIA PETER MATUKIO DAIMA App, DAR
Jeshi la Polisi nchini lipo kwenye mchakato wa kuandaa mageuzi makubwa ya kukifanya chombo hicho kuwa na mwelekea tofauti nawa sasa kwa kubadili fikra kikilenga mahusiano mema na jamii.
Ili kufikia malengo hayo, Jeshi hilo linatarajia kushirikiana kwa karibu na vyombo vya habari ili kuifikia jamii kwa karibu na haraka zaidi.
Hayo yalisemwa juzi Oktoba 18, 2023 na Kamishna Mwandamizi na Msemaji wa Jeshi la Polisi (SACP), David Misime wakati akitoa mada kwenye mdahalo kuhusu umuhimu wa ushirikiano kati ya jeshi hilo na waandishi wa habari jijini Dar es salaam.
Mdahalo huo ulioandaliwa na Taasisi ya International Media Support (IMS) pamoja na Umoja wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) uliwashirikisha waandishi wa habari ambao pia ni wanachama.
Misime alisema kwa sasa jeshi hilo lipo na falsafa ya kutumia Polisi Jamii, kwa lengo la kutambua mchango na kumshirikisha kila mmoja atambue nafasi yake katika Tanzania kuhakikisha nchi yake inadumisha ulinzi, usalama na mahusiano.
“Sasa hivi tupo na falsafa ya kutumia Polisi Jamii, lengo ni kuweza kutambua mchango wa kuweza kumshirikisha kila mmoja ili atambue nafasi yake katika Tanzania kuhakikisha nchi yake inadumisha ulinzi, na usalama na kimahusiano
Ili falsafa hiyo iweze kufanyakazi vizuri, SACP Misime alisema ni lazima jeshi hilo lishirikine na vyombo vya habari kwakuwa vina mchango mkubwa na mahusiano ya moja kwa moja na jamii kupitia taaluma zao.
“Jeshi la polisi linahitaji zaidi vyombo vya habari hususani pale linapotokea suala la taharuki.
“Jeshi la polisi limetangaza namba mpya ambayo itakuwa inapatikana saa 24 kwa siku zote, namba hii itumike pale tu mtu atakapoona kitu cha tofauti cha kutaharisha usalama wa umma,na sisi tutakuwa tayari na kufika hilo eneo mara moja’’
“Wanahabari wanayo rasilimali watu, vifaa kwa kufikisha taarifa, lakini pia watu wengi wanapenda kupata taarifa kwa wanahabari, Hivyo sisi jeshi la Polisi lazima tuwatumie ili kufikisha ujumbe kwa umma”alisema SACP Misime.
0 Comments