Header Ads Widget

SIMBA, SINGIDA FOUNTAIN GATE SC, AZAM KUUNGANA NA TAASISI YA THAMANI WOMEN TANZANIA KUPINGA UKATILI

 



Na fatma Ally, Matukio DaimaApp, Dar 


Naibu Waziri wa Michezo, Sanaa na Utamaduni Hamis Mwijuma amezitaka timu za mpira wa miguu nchini kuungana kuisaidia jamii katika mambo mbalimbali ya kijamii ikiwemo kukemea vikali vitendo vya ukatili wa kijinsia ili kuwa na Taifa imara na lenye maendeleo Jumuishi.


Akizungumza na waandishi  wakati wa ufunguzi wa kampeni ya kupinga ukatili dhidi ya wanawake na watoto kupitia mchezo wa mpira wa miguu ambapo Club tatu za mpira wa miguu za Simba SC,Singida Fountain gate SC na Azam Sc zimeungana na Taasisi ya Thamani Women Tanzania katika kupinga ukatili.


Mwijuma amesema Michezo imekuwa na uwezo wa kuwaunganisha watu na jamii na ina nguvu kubwa katika miktadha yote na kuwaunganisha Kuanzia watu wa kiwango cha taaluma ya juu kabisa mpaka chini, watu wenye vipato tofauti, matabaka na dini tofauti.



Ameongeza "Jambo hili linapelekea mpira kuwa zaidi ya mchezo bali zana muhimu ya kuvunja vizuizi vya kijamii na kitamaduni nje ya uwanja, wachezaji kutoka nyanja mbalimbali wana jukumu la kufanya kazi pamoja kufikia lengo moja, ushindi dhidi ya timu pinzani, mabibi na mabwana, leo tuna-shuhudia vilabu hivi vitatu vikiungana dhidi ya mpinzani mmoja Ukatili".


"Kwa Kipindi kirefu sana swala la kupinga ukatili limekuwa likiongelewa na wanawake, ni wakati muafaka wa sisi vijana wa kiume,kina baba wa makamu tofauti tulijadili hili janga la kitaifa ili turithishe watoto wetu taifa lenye utulivu, amani,upendo na maendeleo"amesema Naibu Waziri Mwijuma.


Amesema kuwa, wanawake wana mchango mkubwa sanaaa katika maendeleo ya taifa la Tanzania na maendeleo yetu wanaume kwa ujumla, huku akiona FIFA na mashirikisho tofauti ya mpira duniani yakitumia mchezo wa mpira kutetea haki za binadamu hivyo amewapongeze sana THAMANI WOMEN TANZANIA kwa kutumia michezo kupaza sauti dhidi ya ukatili wa kijinsia".




Kwa upande wake,  Mkurugenzi Mkuu na mwanzilishi wa Taasisi ya THAMANI amesema kampeni hiyo inalenga vijana wa jinsia ya kiume kuanzia umri wa miaka 13 na wanaume wa makamu kwa kuwashirikisha wanamichezo kupaza sauti kupinga ukatili wa kijinsia wanaimani wanaume watasikia kwani ndio mashabiki wakubwa wa mpira. 


"Ni lazima Vijana wa kiume watambue ya kwamba katika janga hili wao ni suluhu na sio tatizo tu kwahivyo ni muhimu wajadili tatizo hili.The male youth must understand that they are part of the solution not the problem,hence it is key that they have this conversation. Ukatili sio ujanja, ni udhaifu...wanaume wanajukumu la kulinda na kuhudumia sio kupiga na kuumiza, piga mpira sio Mwanamke".


"Amani ya watoto wako ya sasa na baadae inaanza na amani ya mama na utulivu wa nyumbani. Na kwa sasa niseme Kampeni ya kupinga ukatili wa kijinsia ya PIGA MPIRA SI MWANAMKE imezinduliwa rasmi". Amesema Nafue.



Nae,  Mkurugenzi Mtendaji wa Simba Sc, Imani Kajula amesema ukatili wa kijinsia unapaswa kukemewa na watu wote, hivyo amewataka mashabiki wa Simba Sc kupaza sauti zao na kutokuwa miongoni mwa watu wanaofanya vitendo vya unyanyasaji kwa wanawake na watoto.


"Michezo ina njia ya kuunda hali ya jamii kwa wale waliounganishwa kwa shauku hiyo, kwa mfano, ukifuatilia Soka la hapa Tanzania na hata ligi za nje , unaweza kuona jinsi mashabiki walivyo na uwezo wa kushikamana mara moja na shabiki ambaye wamekutana naye hivi karibuni wa timu moja"

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI