Na Matukio Daima Media,Mbeya
ALIYEKUWA Askari polisi J. 2596 Kostebo Samweli Kaziyote (24) wa kituo kikuu cha polisi Mbeya amejiua kwa kujipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake.
Kwa mujibu wa Kamanda wa Polisi mkoani Mbeya, Benjamin Kuzaga amesema kuwa tukio hilo limetokea Octoba 2 mwaka huu majira ya saa 2.15 usiku huko maeneo ya mtaa wa Mzumbe Forest ya zamani.
Kamanda Kuzaga amesema kuwa askari huyo alijipiga risasi kidevuni na kusababisha kifo chake hapo hapo
Hata hivyo Kamanda Kuzaga amesema uchunguzi wa awali umebaini kuwa chanzo cha tukio hilo ni mzozo uliotokea baina yake na mpenzi wake baada ya marehemu kuacha lindo la Benki na kisha kuondoka na silaha bunduki kwenda nyumbani kwa mpenzi wake huyo na kujipiga risasi.
Kufuatia tukio hilo jeshi la polisi mkoa wa Mbeya linaendelea na uchunguzi kuhusiana na tukio hilo .
MWISHO
TANGAZA LA MATUKIO DAIMA ☎️0754 026 299
🍽️KARIBU DODOMA KARIBU MIDLAND INN VIEW HOTEL PIGA 0744788889/0763255550/0676366621
🍽️UWAPO MJINI IRINGA KARIBU LUMILO CLASSICAL HOTEL ☎️0756565603
💅NEEMA BEUATY SPA SALOON IRINGA TUPO KIWANGO KWA GHARAMA NAFUU ☎️0755359989
0 Comments