Zaidi ya kilo 870 za korosho chafu zakamatwa katika ghala Kitandi AMCOS Wilaya ya Nachingwea mkoani Lindi.
Akidhibitisha kukamatwa Kwa korosho chafu mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo alisema kuwa wamemakata korosho chafu ambazo zinadhaniwa kutoka wilaya za jirani na wilaya hiyo ambazo zinataka kuharibu soko la korosho za Nachingwea.
Moyo alisema kuwa kitendo hicho kinafanana na uhujumu uchumi Kwa Taifa na wilaya ya Nachingwea hivyo serikali haiwezi kuwavumilia watu ambao wanahujumu uchumi wa taifa.
Hata hivyo Mkuu wa wilaya ya Nachingwea Mohamed Hassan Moyo ameliagiza jeshi la polisi kumsaka mkulima huyo aliyepeleka korosho chafu kwenye ghala la Kitandi.
0 Comments