Na Fatma Ally, Matukio DaimaApp
Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana CCM (UVCCM) Komredi Mohammed Ali Kawaida (MCC) amemtaka Katibu Mkuu Fakii Raphael Lulandala (MNEC) kuandaa mpango maalum wa ukaguzi wa utekelezaji wa Ilani katika sekta za vijana nchi nzima kwa haraka na kupewa taarifa maalum juu ya hilo, ili vijana kote nchini waone jinsi Serikali yao ilivyowatumikia.
Rai hiyo ameitoa jijini Dar es Salaam, alipokua katika mkutano ulioandaliwa Umoja huo wa kumpokea Katibu Mkuu wa UVCCM Fakii Raphael ambapo amesema Serikali yaJamhuri ya Muungano wa Tanzania na Serikali ya Mapimduzi ya Zanzibar zimetimiza kila aina ya wajibu wa kuwawezesha na kuwajengea mazingira yaliyobora na rafiki kiutumishi.
Aidha, amemtaka pia kuandaa mpango na kushusha maelekezo kwa watendaji na Viongozi wote wa UVCCM Mikoa hadi Matawi kwamba kutoka sasa wajishughulishe na utatuzi wa kero, Changamoto na kuwasemea vyema kuwatetea vijana katika makundi mbalimbali katika maeneo walipo, wakiwemo Maafisa usafirishaji, wamachinga, wavuvi, Wakulima, Wajasiriamali, Mama lishe Vijana, Wanafunzi wa Vyuo na Shule za Sekondari, Wasanii na Wanamichezo.
Amesisitiza kuwa kutoka sasa watakuwa na makundi hayo, na kubeba changamoto zao na kwenda nazo panapostahili kwa utatuzi, na taarifa zao za kazi hizo wazipeleke ofisini hasa katika maeneo ambayo wahusika wameshindwa kuyashughulikia, ili yeye azishughulikie.
Hata hivyo, amewataka viongozi Vijana wote nchini walioaminiwa na Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania wajiandae kukaguliwa namna wanavyotenda na kuenenda pamoja na kuziishi imani walizopewa na wakibainika kuangusha chama nao wataangushwa.
“Sasa leo katika uzinduzi huu wa kishindo cha UVCCM kuelekea 2024/2025 sitaki tena kuendelea kuona wala kusikia vijana wenzetu wa kitanzania wakilalamika kwasababu yenu nyinyi mliopewa dhamana ya kuwatumikia, lakini mmekuwa hamuwatumikii ipasavyo, nasisitiza huu ndio ugomvi wetu sisi UVCCM na wote wanaoshindwa kutimiza wajibu wao katika kuwatumikia Vijana nchini Amesema Kawaida.
Sambamba na hayo amesema anataka kuona Chipukizi iliyo hai, iliyo imara yenye uwezo na inafanyia kazi zake katika kikundi ambapo amesema kiu ya Rais Mama Samia anatamani kuona uhai wa Chipukizi hivyo kuagiza uwepo wa mpango wa Wiki ya Chipukizi Kitaifa.
"Viongozi katika Sekta ya Vijana katika eneo hili unaweza ukawa wewe sio kijana lakini ilimradi umekabidhiwa jukumu la kuwatumikia Vijana, kwanza tuwapongezeni maana wengi wenu mnafanya kazi kubwa na nzuri lakini pia wapo wachache ambao wanasababisha malalamiko na manung’uniko kwa Vijana wenzetu wanaotegemea huduma kutoka kwao hivyo hatutasita kushughulika nao" Amesisitiza Kawaida.
0 Comments