Header Ads Widget

C.W.T WILAYA TANGA WATAKIWA KUWAPUUZA WAPOTOSHAJI



Na Mbaruku Yusuph, Matukio Daima APP Tanga. 


CHAMA cha Walimu Wilaya ya Tanga (CWT)kimetakiwa kuwadharau wanaowapotosha na watambue wanaofanya hivyo wanamaslahi yao binafsi tofauti na Walimu hao.


Kauli hiyo imetolewa na Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga Abdurahman Shiloo wakati wa bonanza la michezo la kuadhimisha ya siku ya Walimu Duniani ambayo inafanyika Oct 5 kila mwaka.


Shiloo alisema Chama hicho cha walimu kipo na kinamaslahi mapana ya walimu ingawa wapo baadhi ya watu wanaweza kukitumia vibaya kwa maslahi yao tofauti na azma ya kuanzishwa chama hicho ambacho ni mtetezi kwa walimu hao.


Aidha alisema umoja wa walimu hao ndio nguvu yao na watambue kuwa sio rahisi kuwa na nguvu kwenye Chama chenu ikiwa ndani yenu kuna watu wanawatenganisha ili msiweze kufikia malengo yenu mliojiwekea.


"Niwaeleze ukweli kwamba nyie ndio moyo wa Nchi na Jamii na tutaendelea kuishauri Serikali kuiangalia sekta hiyo hasa katika swala zima la maslahi yenu"Alisema Meya.

Abdurahman Shiloo, Mstahiki Meya wa Halmashauri ya Jiji la Tanga


Kwa upande wake katibu wa Chama hicho cha Walimu Wilaya ya Tanga Godfrey Rumba alisema dhumuni la kufanya Tamasha hilo la michezo ni kupata muda wa kukusanyika kwa pamoja na kuweza kutoa hoja zao dhidi ya Serikali juu ya kutambua wajibu wao kwa walimu hao ambao ndio chachu katika sekta ya elimu.


Rumba alisema Serikali inapaswa inatimiza stahiki za walimu hao ambao bado hajipewa kipaumbele na kuongeza kuwa katika Tamasha hilo kutakuwa na michezo mbalimbali kama mpira wa miguu,kufukuza kuku,mpira wa Pete,na kuvuta kamba.


Tatu Omari ambae ni katibu wa kitengo cha walimu wanawake Tanga Jiji alisema bado walimu wanakiwango kidogo cha mshahara kisichokuwa na motisha wa aina yoyote na kupelekea kuishi kwa mashaka na kushindwa kukidhi maisha yao mbali ya gharama za maisha kupanda kila siku.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI