![]() |
Patrobas Katambi, Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu |
Na Hamida Ramadhani Matukio Daima APP Dodoma
NAIBU Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu Patrobas Katambi amelitaka Shirika la Viwango Tanzania (TBS) kutoa ithibati ya bidhaa wanazozalisha Vijana wajasiriamali kwa wakati ili kuwaendeleza na kukuza uchumi wa Taifa.
Katambi ametoa agizo hilo Jijini Dodoma wakati akifunga mdahalo kuhusu vijana na uwekezaji kwenye sekta ya kilimo ulioandaliwa na bodi ya wadhamini na Menejimenti ya Taasisi ya Uboreshaji wa Mifumo ya Masoko (AMDT).
Amesema katika maeneo mengi ambayo ametembelea, TBS imekuwa ikilalamikiwa kutowafikia vijana wajasilimali kwa wakati na kutoa mashariti magumu ambayo yanachukua muda mrefu hivyo watoe elimu ya namna ya kufikiwa ili bidhaa wanazozitengeneza zipatiwe vipimo kwa wakati.
Aidha, Mhe. Katambi amesema Serikali imeanzisha mafunzo ya kilimo cha kisasa ambapo jumla ya Vijana 13,088 wamepatiwa mafunzo kati yao vijana 12,580 ni wa mafunzo ya kilimo kupitia teknolojia ya kitalu nyumba, vijana 234 ni wa mafunzo ya kunenepesha mifugo, vijana 200 ni wa mafunzo ya ufugaji samaki na viumbe maji, na vijana 74 ni wa kilimo cha mazao kwa njia ya vizimba.
Kwa upande wake Mwakilishi wa Mkurugenzi Mkuu na Meneja Miradi,Ufuataliaji na Matukio (AMDT) Athuman Zuberi amesema lengo la Mdahalo huo wa Vijana na Fursa kwenye sekta ya Kilimo ni kuwakumbusha ili waweze kuchangamkia Fursa zilizopo kwenye sekta ya Kilimo .
Amesema Serikali ya awamu ya 6 chini ya uongozi wa Rais Samia Suluhu Hassan imewekeza nguvu nyingi kwenye Kilimo lengo Vijana kujikita kwenye Kilimo.
"Ukweli ni kuwa Vijana wengi hapa nchini wamebweteka na hawazitambui fursa zilizopo kwenye Kilimo hivyo ni wakati wa Vijana kujikita kwenye Kilimo na ndio maana AMDT leo tuko Dodoma, " Amesema
MWISHO
0 Comments