Header Ads Widget

WANYABIASHARA WATAKIWA KUTOA RISITI ZA KIELEKTRONIC

 



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR


WAKATI Serikali ikiendelea kuhamasisha Wananchi kudai na kupokea Risiti wanapofanya Manunuzi mbalimbali, Katibu wa Kamati Maalum ya NEC Idara ya Siasa na Uhusiano wa Kimataifa  wa Chama cha Mapinduzi CCM Zanzibar, Khadija Salum Ali amewataka wafanyabiashara kuhakikisha wanatoa risiti za kielektroniki ili kusaidia kodi ya serikali katika kuchochea ukuaji wa uchumi.

Wito huo ametoa wakati akifungua Duka la vifaa mbalimbali kwa kutumia  Umeme la Wawekezaji wazawa wa kampuni  ya Biggie  Eletronik lililopo Michenzani Mall Mjini Unguja ambapo ameeleza kuwa utoaji wa risiti za Kieletronic inachangia ukuaji wa uchumi wa Nchi.



Amesema ni wajibu wa kila mfanyabiashara kutoa risiti ya kieleketroniki wakati wa kufanya mauzo ili kodi stahiki ya serikali iweze kukusanywa na kuchochea maendeleo ya nchi.

"Serikali inaendelea kuhamasisha wananchi kudai risiti hivyo ni wajibu wenu kama Wafanyabiashara sasa kuwa mstari wa mbele katika kutoa risiti za Kieletronic ili kuchochea Maendeleo endelevu," Amesema.

Kwa upande wake Afisa Mtendaji mkuu na muanzilishi wa kampuni ya Biggie Elektronik  Hamed Salum amesema uwekezaji huo utahakikisha unatoa fursa mbalimbali kwa wannachi wa Zanzibar ikiwemo kutoa ajira na kuhakikisha kodi ya serikali inapatikana kwa kiwango stahiki.

"Tumepokea maelekeezo yaliyotolewa na tutahakikisha tunatoa na kuhamasisha kwa wafanyaboashara wengine kutoa risiti ili kuchochea maendeleo ya Zanzibar yetu," amesema.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI