NA HADIJA OMARY,MATUKIO DAIMA APP,
LINDI
Watu 7 wamefariki dunia na wengine 22 wamejeruhiwa katika ajali iliyohusisha basi la namba T.604 DJJ aina ya Scania mali ya kampuni ya Saibaba linalofanya safari zake Nachingwea kwenda Dar es salaam kugongana na na gari namba T 217DXG aina ya Tata Bus mali ya kampuni ya Baharia linalofanya safari zake Dar es salaam kwenda Tandahimba.
Ajali hiyo imetokea Oktoba 5 huko katika kijiji cha Kiwawa Wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Kamanda wa Polisi Mkoa wa Lindi ACP PILI MANDE amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo akisema chanzo ni derva wa basi la kampuni ya Saibaba kutaka kulipita gari kubwa la mizigo ambalo lilikuwa mbele yake na ndipo walikutana na basi hilo dogo la kampuni ya Baharia likitokea Dar es salaam na kugongana uso kwa uso.
Amewataja Waliofariki dunia ni, Lucas John (59) dereva aliyekuwa akiendesha basi la kampuni ya Saibaba pamoja na Omari Alli Abdalah (49) ambaye ni dereva wa gari ndogo ya kampuni ya Baharia na kwamba Miili ya marehemu 5 bado haijatambuliwa majina yao na Majeruhi 3 ambao hali zao ni mbaya majina yao hayajafahamika kati yao wanawake 2,mtoto mdogo jinsia ya kiume 1 wamelazwa katika hospitali ya Kinyonga wilaya ya Kilwa.
Kamanda Mande amesema pia Majeruhi wengine 19 wanaendelea kutibiwa na kuangaliwa hali zao na madaktari na wataruhusiwa kutegemeana na hali zao za unafuu huku akitoa wito kwa madereva wote kufuata sheria za usalama barabarani na kuwa makini na kipindi mvua inapokuwa inanyesha kwa kuwa barabara inakuwa inateleza.
Kwa upande wake Mganga mkuu wa halmashauri ya kilwa Dkt. Lusajo Mwakajoka amethibitisha kupokea majeruhi 22 kati yao wanawake 11na wanaume 11 ambao kati yao wawili ni watoto huku watatu kati yao wakiwa na majeraha makubwa katika maeneo ya kichwani
" hawa ni wanaume wawili pamoja na mtoto mdogo wa kiume ambae mpaka sasa mama yake bado hajatambulika japo tinahisi mama yake uwenda atakuwa ni marehemu ambao walifaliki kwenye ajali ile"
Alisema licha ya kupokea majeruhi hao wamepokea pia miili ya marehemu saba ambapo kati yao wanaume walikuwa wanne na wanawake mmoja pia na watoto wawili wakiume mmoja na wakike mmoja na miili yao tayari imehifadhiwa kwenye chumba cha kuhifadhia maiti.
0 Comments