Header Ads Widget

WATAKAO WAKWAMISHA DARASA LA SABA KUFANYA VIZURI NJOMBE KUSHUGHULIKIWA

 

Mwenyekiti wa Halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete

Baadhi ya wanafunzi Halmashauri ya mji wa Njombe

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE

Onyo limetolewa kwa wazazi wilayani Njombe kuepukana na tabia za kuwashawishi wanafunzi wasifanye vizuri mitihani yao ya mwisho ili kuwatumikisha kwenye kazi za ndani na kwamba hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.


Hatua hiyo inakuja kufuatia wanafunzi wa darasa la saba kutarajia kuanza mtihani wao wa mwisho septemba 13 na 14 mwaka huu nchini kote na kwamba mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Njombe Mhe.Erasto Mpete anawataka wazazi kuacha fikra potofu za kuzuia watoto wasifanye vizuri huku akiwaonya walimu wenye nia ya kufanya udanganyifu kwenye mitihani.


Kwa mujibu wa afisa elimu msingi halmashauri ya mji wa Njombe mwalimu Fider Kiharamba Jumla ya wanafunzi 4871 wanatarajia kufanya mtihani wa mwisho wa kuhitimu elimu ya msingi.


Aidha baadhi ya wazazi mjini Njombe akiwemo Augustino Mtweve na Christina Luoga wamekiri kuwapo kwa baadhi ya wazazi wenye tabia ya kuzuia watoto wao wasifanye vizuri katika mitihani yao ili kwenda kuwatumikisha katika kazi za ndani huku wakiwataka kuacha tabia hiyo.


Kwa upande wao baadhi ya wanafunzi wanaofanya mtihani wao wa mwisho akiwemo Chrispin Luvavila,Frank Mtweve  na Omary Kihombo wamesema wamejiandaa vyema kuelekea katika chumba cha mtihani.


Kituo hiki kinawatakia kila jema katika mtihani wa mwisho  wanafunzi wa darasa la saba mwaka huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI