Na Fadhili Abdallah,Kigoma
WALIMU katika wilaya za Kasulu na Buhigwe mkoani Kigoma wameeleza kuwa huduma ya mikopo inayotolewa na Benki ya NMB ni msaada mkubwa kwao katika kumuendelea mwalim kwenye maisha ya utumishi na baada ya utumishi.
Baadhi ya walimu waliohudhuriwa kongamano hilo walisema hayo katika kongamano la siku ya Mwalimu lililoandaliwa na Benki ya NMB na kushirikisha walimu zaidi ya 200 kutoka kwenye wilaya hizo.
Mwalim Rebeka John kutoka shule ya Sekondary Makere Wilaya ya Kasulu alisema kuwa huduma ya Mwalimu Spesho iliyoanzishwa na Benki ya NMB imeleta faraja kubwa kutokana na mahitaji ambayo walimu wanayo ikiwemo mkopo wa elimu unaotozwa asilimia tisa ya riba.
Alisema kuwa Mwalimu anaweza kukopa hadi shilingi milioni 10 kwa mkopo huo kwa riba ya asilimia tisa jambo ambalo linaweza kutoa fursa kubwa kwa walimu kujiendeleza kwenye masomo ya elimu ya juu kutokana na walimu wengi kuwa wameshapita kigezo cha kupata mkopo kutoka bodi ya mikopo ya elimu ya juu hivyo inakuwa rahisi kujiendeleza kupitia mkopo wa mwalimu spesho.
Naye Mwalim Mussa Kanyoe Afisa elimu Taaluma halmashauri ya wilaya Kasulu alisema kuwa mikopo ya Pikipiki,bajaji na shughuli za kilimo zinaweza kuwa mkombozi mkubwa kwa walimu kuwa na kitega uchumi ambacho kitaendelea kumuingizia kipato hata anapomaliza muda wake kwenye utumishi wa umma.
Akifungua kongamano hilo Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Mji wa Kasulu,Dolla Kusenge amewaasa walimu kujihadhari na mikopo umiza inayotolewa na zisizozingatia sheria na sera za mikopo za benki kuu mikopo hiyo ikiwa na riba kubwa ambazyo zimeathiri maisha na utendaji kazi wa walimu.
Kusenge alisema zipo taasisi zinazotoa mikopo ambazo licha ya kuwa na riba kubwa lakini zimekuwa na masharti magumu ikiwemo kushikilia kadi za benki za walimu urataibu ambao haukubaliki kwa namna yeyote.
Akizungumzia kongamano hilo la siku ya Mwalim Meneja wa kanda ya Magharibi wa benki ya NMB, Vicent Urio alisema kuwa kongamano hilo limeandaliwa maalum kwa ajili ya kupata mrejesho wa walimu kuhusiana na huduma kwa walimu maarufu kama Mwalim Spesho zilivyowezesha kuwafikia walimu na changamoto zilizojitokeza.
Urio alisema kuwa mkutano huo umeandaliwa kupata maoni ya walimu hao ili kuona namna ya kupata masuluhisho kulingana na changamoto zilizojitokeza na nini kifanyike kuboresha huduma kwa walimu hao ikiwemo mikopo ya aina mbalimbali ambayo haikuwa inatolewa na benki nyingine nchini ikiwemo mikopo ya kilimo, vyombo vya usafiri kwa ajili ya biashara (Pikipiki,Bajaji) na mikopo kwa ajili ya shughuli za uvuvi.
0 Comments