Na Elizabeth Ntambala Rukwa
Mganga mkuu wa mkoa Ibrahim Isaack amewataka wananchi kushiriki kikamilifu katika zoezi la utoaji wa chanjo kwa watoto chini ya miaka 8 ili kujikinga dhidi ya ugonjwa wa Polio.
Kauli hiyo imetolewa leo wakati wa uzinduzi wa kikao cha Waandishi wa habari juu namna ya kujikinga pamoja na kutoa elimu kwa wananchi juu ya ugonjwa wa polio
Aidha Mganga mkuu lsack amesema kuwa kila mtoto wa mkoani Rukwa anapaswa kupata chanjo ya polio kwani itaongeza kinga mwilini na kumuepushia mtoto ulemavu wa kudumu au hata kifo kwani ugonjwa huo hauna tiba.
Amesisitiza kuwa wazazi wanatakiwa kuto waficha watoto ndani ili waweze kupata haki zao za kuwa na afya njema na kuacha mila potofu kwani kufanya hivyo kutaleta madhara makubwa katika jamii.
Kwa upande wake Mratibu wa chanjo mkoa Ndenisia Ulomi amebainisha kuwa malengo ya Mkoa wa Rukwa ni kuwafikia watoto 391,883 kwa kuwapatia chanjo aina ya pili ya polio katika vituo vya Afya na nyumba kwa nyumba. Ndenisia amewataka wananchi kutoa taarifa za viashiria vya ugonjwa wa polio katika kituo cha afya iwapo dalili za mtu mwenye viashiria vya polio ikionekana ili iwe rahisi kuudhibiti.
0 Comments