Header Ads Widget

UVCCM MOSHI VIJIJINI NYUMBA KWA NYUMBA KUSAKA KURA..

Na Gift Mongi MATUKIODAIMA APP MOSHI.

Baada ya kuzinduliwa rasmi Kwa kampeni za uchaguzi mdogo wa diwani katika kata ya Old Moshi Magharibi hapo septemba 3.2023 tayari baadhi ya makada wajigawa kuhakikisha ushindi unapatikana chama cha mapinduzi(CCM).

Miongoni mwa makada waliojitokeza kuusaka ushindi huo nyumba kwa nyumba mlango kwa mlango ni pamoja na mwenyekiti wa UVCCM wilaya ya Moshi Vijijini Yuvenail Shirima ambapo amesema wanausaka ushindi na sio kusubiria ushindi wa bahati nasibu.

'Hatulali na hakuna nyumba au mlango ambao tutauacha bila kubisha hodi katika kwenda kusaka kura kwani hataegemei kupata ushindi wa mashaka'anasema mwenyekiti huyo na kuongeza

'Utaona kama hii leo tupo hapa katika tawi la Mande na matawinyote utaratibu wetu utakuwa ni hivi hivi hadi tutakapomaliza kampeni tuwe tumemfikia kila mtu na kila nyumba na pia kwenye kila mlango'anasema

Gerson Onesmo mkazi wa Old Moshi anasema kuwa kampeni zinazoendeshwa na CCM zimekuwa za kistaarabu na kuwa ni ukomavu wa siasa na wananchi kwa sasa hawataki porojo wanataka maendeleo.

'Tunaenda kuendelea pale tulipoishia na sasa niwahakikishie kata yetu inaenda kurudi katika mikono salama'anasema

Menyasumba Macha alikuwa diwani wa tatu wa CCM Mkoa wa Kilimanjaro kupoteza maisha na kufanya idadi ya kata zilizoko wazi kufikia tatu, kata hizo ni pamoja na Old Moshi Magharibi (Moshi), Kalimawe na Njoro (Same).

Tayari chama cha mapinduzi (CCM)kimeshazindua kampeni zake katika kata husika na kuwa wamejipanga kuhakikisha kata zote hizo zinarudi katika mikono yake kwani hapo awali' zote zilikuwa chini ya chama hicho

MWISHO.








Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS