Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Serikali mkoani Njombe imeombwa kuingilia kati changamoto ya uhaba wa mafuta unaosababisha athari kubwa za kiuchumi na usafirishaji kwa wananchi.
Kutokana na kuadimika kwa Mafuta ya Petrol na Dizel Mkoani Njombe Watumiaji wa bidhaa Hiyo Wamesema kuwa Shughuli nyingi za Kiuchumi zimesimama na Hivyo kuathiri Vipato vyao vya Kila siku.
Mapema asubuhi Kituo hiki kimeshuhudia Msongamano mkubwa wa watu katika Vituo mbalimbali vya Mafuta Mjini Njombe ambapo baadhi ya Watumiaji wa Bidhaa hiyo ambayo kwa sasa imekuwa adimu akiwemo George Maltin Wamesema kuwa Uhaba wa Mafuta umesababisha Shughuli nyingi za Kiuchumi kuyumba.
Kufuatia Uhaba Huo Wauzaji wa Mafuta Mkoani Njombe akiwemo Octavian Joseph Wamesema Bidhaa Hiyo imekuwa adimu kwa sasa na Sio kwamba Wao Wamekuwa Wakificha Mafuta kama Baadhi ya Watu Wanavyosema.
Kwa upande wake Katibu Tawala Wilaya ya Njombe Agatha Mhaiki baada ya kufanya ukaguzi kwenye vituo mbalimbali vya mafuta wilayani hapa amekiri kuwepo kwa Uhaba wa Mafuta na Kwamba tayari Wamesha ripoti Changamoto Hiyo katika mamlaka husika.
Kila Jumatano ya mwanzo wa mwezi Mamlaka ya nishati na maji Nchini EWURA hutangaza bei mpya ya mafuta iwe kupanda ama kushuka jambo ambalo wengi wanaamini baada ya kutangazwa mafuta huenda yakaanza kupatikana.
0 Comments