Na WMJJWM, Dodoma
Katibu Mkuu Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wanawake na Makundi Maalum Dkt. Seif Shekhalage amewasili katika ofisi yake mpya na kukabidhiwa majukumu na aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara hiyo Dkt. John Jingu Sept 4, 2023.
Tukio hilo limekuja kufuatia mabadiliko yaliyofanywa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzanja Mhe. Dkt. Samia Suluhu Hassan yaliyohusisha Baraza la Mawaziri na Makatibu Wakuu na Manaibu Makatibu Wakuu hivi karibuni.
Akizungumza na Menejimenti ya Wizara, Dkt. Shekhalage ametoa wito kwa watumishi wote kushirikiana ili kufikia lengo la kuwahudumia wananchi.
"Nitakuwa tayari kupokea maelekezo ya Mhe. Waziri, niwahakikishie kuwa mimi nitakuwa mtumishi mwenzenu, tutafanya kazi kwa umoja na ushirikiano" alisema Dkt. Shekhalage
Kwa upande wake Dkt. John Jingu ameishukuru Menejimenti na watumishi kwa ushirikiano waliompatia kwa kipindi chote alichofanya kazi Wizarani hapo.
Naye Waziri Mhe. Dkt Dorothy Gwajima akizungumza wakati wa hafla hiyo fupi, amesema lengo la Mheshimiwa Rais kufanya mabadiliko hayo ni jema ili kuendelea kuwatumikia watanzania.
Amemshukuru Dkt. Jingu kwa utendaji wake akiwa Wizarani hapo na kumtaka ashirikiane vizuri na Katibu Mkuu Dkt. Shekhalage katika utendaji kwani Wizara hizo zinategemeana.
"Wizara ya Maendeleo ya Jamii ikifanya vizuri kwenye Jamii hata kwenye Hospitali zetu wagonjwa watapungua" amefafanua Waziri Dkt. Gwajima.
0 Comments