Header Ads Widget

TAASISI YA UMOJA WA AMANI-KWANZA WATAKIWA KUHUBIRI AMANI KUANZIA NGAZI ZA MSINGI.

Na Fredrick Siwale - Matukio Daima App Dodoma.                            


TAASISI ya Umoja wa amani kwanza ( UAK) imetakiwa kushuka chini kuihubiri amani kwa kutoa elimu ya amani na uzalendo kuanzia shule za msingi, Sekondari na Vyuo ili kutengeneza kizazi chenye kuilinda amani.                                    



Rai hiyo imetolewa na mkuu wa Wilaya ya Kondoa Bw.Hamisi Mkanachi ambaye alimwakilisha mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi.Rosmary Senyamle kwenye maadhimisho ya siku ya amani Ulimwenguni ambayo kwa Tanzania siku hii inaadhimishwa kila ifikapo septemba 21 kila mwaka.                         


Mkuu wa Wilaya ya Kondoa   Bw.Mkunachi kupitia hotuba ya mkuu wa mkoa wa Dodoma Bi.Senyamle alisema maadili mema yanaanzia kwa mtu mmoja mmoja ndani ya familia  hivyo iko haja kufika hadi kwa Watoto wa mitaani.

Alisema UAK inao wajibu wa kujitanua  zaidi kuanzia chini kabisa hapa Nchini na ikipendeza sana iendelee kuvuka kama  zilivyofikiwa Nchi za Uganda na Burundi.        


" Ikumbukwe kuwa Nchi hii ina Watu zaidi ya milioni 61 kwa Taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza kuwa Wanachama laki tatu haipendezi hamasisheni Wananchi kujiunga na Taasisi yenu." Alisema Bw.Mkunachi.                    


Upande wake raisi wa Taasisi ya umoja wa amani kwanza Tanzania ,Afrika na Ulimwenguni kote Dr.Wilson George Munguza ,alisema anamshukuru sana Mh.Dr.Samia Suluhu Hassan Raisi wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano kwa kuendelea kuilinda "TUNU YA TAIFA YA AMANI katika kipindi chote cha Uongozi wake hadi sasa.               

Dr.Munguza alisema Taasisi ya Umoja wa amani kwanza kwa niaba ya Watanzania inamshukuru na kumpongeza na kumuahidi kumsaidia na kuhakikisha TUNU HII YA AMANI katika Taifa la Tanzania ,Afrika  na Dunia inapewa kipaumbele na uzito unaostahili wakati wote.                                  


" Taasisi ya Umoja wa Amani Kwanza ni taasisi isiyo ya faida ambayo haihusiki na chama chochote cha kisiasa ,dini wala dhehebu lolote,Wala jinsia na imesajiliwa kisheria  chini sheria ya asasi sura 337 ,R.E 2002  .                               


Dr.Munguza alisema lengo kuu la taasisi ya umoja wa amani kwanza ni " Kuhamasisha na kutoa elimu kwa Wanachama na wasio na Wanachama ,ndani na nje ya Nchi kuhusu kutunza na kuhamasisha amani  duniani"      

                        

Akihitimisha Dr.Munguza alisema kwa sasa Taasisi imefanikiwa pia kuanzisha matawi nje ya Nchi kw sasa taasisi ya umoja wa amani kwanza ina matawi manne kutoka mataifa mbali mbali yakiwemo  Kenya,Uganda, Burundi na Rwanda.        


Upande wake mkuu wa mafunzi wa mafunzo kwa makampuni binafsi ya Ulinzi kutoka makao makuu ya Polisi Nchini, ACP.Elisante Ulomi aliwataka Umoja wa amani kwanza kuendelea kuwa kinara wa utunzaji wa amani na iwe sehemu ya jicho la Serikali kwa kufichua viashiria vya uvunjifu wa amani.           


" Umoja wa amani kwanza msikalie taarifa wala msizifiche ili kwa pamoja tushiriki kuilinda amani hii iliyopo " Alisema ACP.Ulomi. 




















Matukio ya picha mbali mbali katika maadhimisho hayo ya siku ya amani Duniani ambayo yamefanyika Jijini Dodoma katika ukumbi wa Kilimani kwa kushirikisha Wanachana wa umoja wa amani kwanza kutoka mikoa yote ya Tanzania bara na Visiwa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS