Header Ads Widget

MADIWANI NJOMBE DC WATAKA TARATIBU ZIFUATWE UWEKEZAJI WA PARACHICHI IKANG'ASI

Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE


Wakati hamasa ikiwa kubwa katika mpango wa uwekezaji wa kilimo cha parachichi kwenye ardhi ya ekari elfu 89 kwa mujibu mkuu wa mkoa wa Njombe katika kijiji cha Ikang'asi Kata ya Mfiriga wilayani Njombe Baadhi ya madiwani wamelalamikia kutoshirikishwa katika mchakato huo.


Katika kikao cha baraza la madiwani halmashauri ya wilaya ya Njombe baadhi ya madiwani hao akiwemo Innocent Gwivaha na Javan Ngumbuke wamesema suala hilo limekuwa na mwamko mkubwa kupitia mitandao ya kijamii ilihali kama baraza la madiwani halijaidhinisha jambo hilo hivyo wanataka hatua zote zifuatwe.

Hivi karibuni katika mitandao ya kijamii kumekuwa na orodha ndefu ya watu wanaotaka ardhi hiyo kwa ajili ya uwekezaji wa zao la parachichi ambapo Kaimu mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Njombe ambaye ni mwanasheria bwana George Makacha amesema halmashauri hiyo bado haijapitisha chochote juu ya uwekezaji huo hivyo hatua zote zitazingatiwa.


Kwa upande wake mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Njombe Valentino Hongoli amewatoa hofu madiwani hao huku akielekeza wataalamu kulifuatilia kwa karibu jambo hilo.


Mara nyingi mkuu wa mkoa wa Njombe Antony Mtaka amekuwa akilipigia chapuo eneo hilo la uwekezaji wa parachichi ambalo anasema limeshapimwa na litakuwa maalumu kwa zao hilo kama ilivyo katika msitu wa mitu ya mbao wa sao hill Wilaya ya Mufundi mkoani Iringa.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS