Header Ads Widget

MASOUD JUMA APIGA HESABU ZA UBINGWA WA NGAO YA JAMII DHIDI YA JKU.


Na Thabit Madai, Matukio Daima App, Zanzibar.


WAKATI Joto la fainali ya Ngao ya Jamii kati Maafande wa KMKM dhidi ya JKU  ikipanda, makocha na Wachezaji wa timu hizo wametambiana kila moja timu yake kushinda mchezo huo ambao unasubiriwa kwa hamu na Mashabiki wa Soka Visiwani Zanzibar.


Wametoa tambo hizo kufuatia Mkutano na Waandishi wa Habari wakati wa Mazoezi ya Timu hizo katika kiwanja cha Maotsung pamoja na Saateni Mjini Unguja.


Kocha Mkuu wa Timu ya KMKM Masoud Djuma amesema kwamba, mchezo utakuwa mkubwa na mzuri kwa klabu yake hasa kwa mwanzo wa msimu na anajua umuhimu wa mchezo huo kwa kila timu.


Amesema kwamba Matumaini yake kuwa ataibuka na Ushindi na kuwa Bingwa wa ngao ya Jamii ambayo itamjenga na Timu yake Mpya.

"Furaha yangu kubwa ni kucheza mchezo huo na kuwa bingwa wa ngao ya Jamii kwani Timu ya JKU ni kubwa kwa hap visiwani ukizingatia wametoka katika mashindano ya kimataifa na kushinda dhidi ya Singida," amesema.


Kwa upande wake Mchezaji wa JKU ambae ametoka Taifa la Kameroon Engola Martin amesema kwamba pamoja na ugumu wa mchezo huo wachezaji wa JKU wamejipanga na ushindi wa Mchezo huo.


Amesema kuwa anafarajika kucheza katika Klabu ya JKU ambapo ni moja ya timu bora ndani ya Visiwa vya Zanzibar.


Mchezo wa Ngao ya Jamii kati ya KMKM na JKU unatarajiwa kuchezwa Septemba 09 mwaka huu katika Dimba la Maotsung majira ya saa 10 jioni.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



BBC NEWS