Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Ili kuepukana na magonjwa ya mlipuko kikiwemo kipindupindu na magonjwa ya kuhara wananchi mkoani Njombe wametakiwa kuacha tabia ya kutupa taka ngumu kwenye mabonde yanayotiririsha maji.
Agizo hilo limetolewa na Afisa Afya wa mkoa wa Njombe Saada Milanzi katika zoezi la ufanyaji usafi lililojumuisha mamia ya wakazi wa halmashauri ya mji Njombe katika mtaa wa National Housing.
Aidha Enosy Lupimo Ofisa Mtendaji wa Kata ya Njombe Mjini ambaye anasema wameunda kikosi kazi cha watu watano kwenye kila ubalozi kwa ajili ya kufuatilia suala la usafi huku watakaokaidi kutekeleza agizo la usafi hatua kali za kisheria zitachukuliwa.
Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Njombe, Kuruthum Sadick ameonya tabia ya baadhi ya watu wanaotupa taka hovyo mitaani.
Kwa upande wao baadhi ya wananchi mkoani Njombe akiwemo Zuwena Msemwa wamelaani kitendo cha baadhi ya wanaokwenda kutupa taka kwenye maeneo yasiyostahili.
0 Comments