Header Ads Widget

HALMASHAURI YA RUNGWE YAFANYA VIZURI ZOEZI LA CHANJO YA POLIO

 

Renatus Mchau Mkurugenzi wa Halmashauri ya Rungwe 


HALMASHAURI ya wilaya ya Rungwe imefanya vizuri katika zoezi la chanjo ya polio ambapo zoezi hili limefanyika katika takribani mikoa   Mitano ya Tanzania bara


Mikoa iliyoshiriki zoezi la chanjo ni pamoja na Mbeya, Katavi, Rukwa, Songwe, Kigoma na Kagera


Rungwe imechanja kwa asilimia 132.40%  huku ikiwafikia watoto walio chini ya umri wa miaka 8 wapatao 114,832 na awali malengo yalikuwa kuchanja watoto 86,732 na hivyo chanjo imevuka malengo kwa asilimia 32.


Rungwe imeshika nafasi ya Pili baada ya Halmashauri ya Chunya huku ikifuatiwa na Mbeya jiji.


Katika zoezi hili Mkoa wa Mbeya umechanja jumla ya watoto  766,850 sawa na aslimia 124.82% 


Mafanikio haya yametokana na ushirikiano mzuri kati ya Wananchi, Kamati ya Ulinzi na Usalama, Watalamu wa afya, Vyombo vya habari na Wadau mbalimbali


Ugonjwa wa POLIO ambao kwa mara ya Mwisho Tanzania ilipata Mgonjwa wake mwaka 1996 hivi karibuni katika hatua nyingine Mgonjwa amegundulika Sumbawanga Mkoani Rukwa.


POLIO NINI?


POLIO ni ugonjwa unaosababishwa na virusi vya polio (poliovirus)


Ugonjwa huu humsababishia Mgonjwa kupooza  viungo vya mwili na hatimaye kifo 


Virusi vinaweza kuingia kwa njia ya mdomo kwa kunywa maji au chakula ambacho kimechafuliwa na kinyesi kutoka kwa mtu aliyeambukizwa na virusi hivyo


POLIO haina tiba lakini inaweza kuzuiliwa kwa kupata chanjo ya polio ya matone au sindano (IPV).


Ikumbukwe kuwa  chanjo ya Polio haina madhara yoyote. Mtoto anaweza kupata chanjo ya polio  mara nne au zaidi ili kuimarisha kinga dhidi ya ugonjwa huu.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI