BAADA ya Kuibuka Taarifa zilizozua Hofu na taharuki juu ya uwepo wa Mtu asie na kichwa katika baadhi ya Maeneo ya ndani ya Mji wa Unguja, Mkuu wa Wilaya ya Magharib B Unguja Hamida Mussa Khamis leo amejitokeza hadharani na kutia kauli juu ya Uvumi wa Taarifa hizo na kiwatoa hofu kuwa hakuna kitu kama hicho.
"Uvumi umekuwa Mkubwa sana kwa baadhi ya maeneo , Miki nataka niwatoe hofu kuwa hakuna kitu hicho kikubwa naendelea na harakati za maisha kama kawaida," Ameeema Mkuu wa wilaya Hamida.
Pia Mkuu wa wilaya Hamida amewataka Wananchi kuendelea kuiomba Taifa ili kujiepusha na Mabalaa kama hayo.
Maeneo ambayo alikuwa nasadikiwa kuwa na Mtu asie kuwa na Kichwa ni pamoja na Tomondo, Kwa Mchina, Chukwani na Meli Nne.
0 Comments