Na Gabriel Kilamlya Matukio DaimaAPP NJOMBE
Waziri wa Utamaduni sanaa na michezo Balozi Dokta Pindi Chana amesema Utamaduni unaodumishwa katika taifa la Tanzania umesaidia Sana kudumisha amani tofauti na mataifa mengine.
Waziri Dkt.Chana ametoa kauli hiyo wakati akizindua Tamasha la Kitaifa la Utamaduni linalofanyika mkoani Njombe na kwamba Wizara yake imeendelea kuwa chachu ya kudumisha amani na kutoa ajira nyingi kwa vijana huku mila na tamaduni mbaya za watu wa magharibi zikitakiwa kupingwa na kila Mtanzania.
Naye katibu mkuu wa Wizara ya Utamaduni Sanaa na michezo Said Yakubu amesema maagizo ya Rais ya kufanyika kwa matamasha haya kunasaidia kuunganisha makabila yote ya bara na visiwani ikiwa ni njia moja wapo ya kurahisisha udumishaji wa mila za kiafrika.
Mwenyekiti wa umoja wa machifu Tanzania Antonia Sangalai Amesema tamaduni zetu za kiafrika ni muhimu kuenziwa kwa kuwa zinasaidia Sana kukabiliana na Changamoto ya mmomonyoko wa maadili.
Kwa niaba ya Mkuu wa mkoa wa Njombe,Mkuu wa Wilaya ya Njombe Kissa Kasongwa amesema wakati tamasha likiendelea wananchi nao wamekuwa wakidumisha Utamaduni pamoja na kuchapa kazi.
Kwa upande wao wakazi wa Njombe akiwemo Rashid Karume na Chifu Ulaya Kayombo wamekiri kuwa Tamasha hilo litawafungulia milango ya kiuchumi huku wengine wakionya kurithi tamaduni mbaya za watu wa Magharibi.
Tamasha la Kitaifa la utamaduni linalofanyika mkoani Njombe kuanzia agosti 25 litahitimishwa agosti 27 mwaka huu.
0 Comments