Header Ads Widget

MRADI WA MAJI WA KUHUDUMIA WATU 8,400 WAZINDULIWA NA MWENGE WA UHURU TANGANYIKA.

 


Na Eliza Ntambala Tanganyika.


WATU 8,400 wa kijiji cha Vikonge na Kitongoji cha Inyagantambo kilichopo katika kijiji cha Majalila Halmashauri ya Wilaya ya Tanganyika Mkoa wa Katavi wameondokana na changamoto ya maji safi na salama baada ya mradi wa maji Vikonge kuanza kuwahudumia


Mradi huo ambao ulianza kutekelezwa katika kijiji cha Vikonge May, 2022 na kukamilika na kuanza kutoa huduma Nov, 2022 umezinduliwa na kiongozi wa mbio za mwege wa uhuru kitaifa,Abdalla Shaib Kaim ambapo gharama za ujenzi wa mradi huo ni  fedha Tshs 608,603,837/= zimetumika.


Meneja wa RUWASA wilaya ya Tanganyika Mhadisi, Alikam Sabuni akitoa leo taarifa ya ujenzi wa mradi wa maji Vikonge mbele ya kiongozi wa mbio za mwege wa uhuru kitaifa Abdalla Shaib Kaim amesema kuwa manufaa ya mradi huo utahakikisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika zahanati ya kijiji cha Vikonge na kuondoa maradhi yatokanayo na matumizi ya maji yasiiyokuwa safi.


Alikam ameeleza kuwa mradi huo unaimarisha mahudhurio ya wanafunzi mashuleni hasa katika shule ya msingi Vikonge pamoja na unarahisisha upatikanaji wa huduma ya maji safi na salama katika soko la kijiji cha Vikonge.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI