Header Ads Widget

KIKOSI CHA USALAMA BARABARANI KUTOA ELIMU KWA KUTUMIA MICHORO INAYOONESHA MIFANO YA BARABARA NA MADARAJA

 


NA CHAUSIKU SAID_MATUKIO DAIMAAPP MWANZA 


Jeshi la polisi Mkoa wa Mwanza kupitia kitengo Cha Usalama barabarani wameanza kutoa elimu Kwa watumiaji wa barabara Kwa kutumia michoro mbalimbali inayoonesha mifano ya uhalisia wa barabara na madaraja.


Akizungumza na makundi ya  madereva  waendesha bodaboda, bajaji, daladala pamoja na wadau wa usafirishaji kwa ujumla Kamanda wa Jeshi la Polisi Mkoani Mwanza Wilbrod Mutafungwa amepongeza ubunifu mkubwa uliofanywa na kikosi cha usalama barabarani Mkoa wa Mwanza.


Ameeleza kuwa wamelenga kuelimisha Watembea kwa miguu na wanaotumia vyombo vya moto ili waweze kutumia barabara kulingana na mazingira ya barabara waliopo.




"Ndio maana tumekuja na mfano wa barabara unaonesha uhalisia wa madaraja yaliyopo katika Barabara zetu za Watembea kwa miguu" Alisema Mtafungwa"



Mtafungwa ameeleza kuwa kumekuwa na changamoto  ya watu kutotumia madaraja ambayo serikali imejenga kwa gharama kubwa na kuanza kupita pembezoni mwa barabara sehemu ambazo haziruhusiwi kupita.



Aidha amefafanua kuwa madaraja hayo ya watembea kwa miguu yamebaki kuwabya kupigia picha na watu wanaokuyana kwa ajili ya kufanya starehe zao badala ya wavuka kwa miguu kwa ajili ya kuvuka na kupunguza uwezekano wa watu kupata ajali.




"Sasa tumekuja na mifano hiyo ya barabara na hivyo tutakwenda maeneo yote ya watembea kwa miguu yakiwemo makanisa, shule pamoja mikusanyiko mbalimbali ya watu, lakini pia na nyie mlippata elimu mkatusaidie kufundisha wengine ili tuweze kupunguza ajali zitokanazo na uzembe" Alisema Mtafungwa.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI