Header Ads Widget

WANANCHI WASHAURIWA KUFANYA MAZOEZI

 



NA THABIT MADAI, ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP


WANANCHI Visiwani Zanzibar wameshauriwa kufanya Mazoezi na kuendelea kula Mlo kamili ili kuimarisha Afya zao na kuepuka uwezekano wa kupata Magojwa yasiyoambukizwa.


Wito huo umetolewa na Waziri wa Afya Zanzibar Nassor Ahmed Mazrui wakati akizungumza na Wananchi wa Jimbo la Chumbuni mara baada ya Matembezi ya Mshikamano yaliondaliwa na Pondeza Foundation ikiwa ni kuelekea tamasha la michezo katika jimbo hilo.


Amesema, Ni Muhimu kwa Wananchi kuzingatia ulaji wa Chakula bora pamoja na kufanya Mazoezi ili kujenga Afya Bora.


"Mimi leo sina Mengi ya Kueleza nataka kuwasisitiza Wananchi Visiwani Zanzibar kuendelea kula Mlo Kamili pamoja na kufanya Mazoezi jambo ambalo litasaidia kuimarisha afya zao na kuepukana na Maradhi mbalimbali," amesema.


Nae Mbunge wa Jimbo hilo Salum Ussi Pondeza ameeleza kuwa, Matembezi hayo ni muendelezo wa Shughuli kuelekea Tamasha maalum la Mchezo katika jimbo hilo ambalo litatoa fursa mbalimbali za Vijana.


"Katika Wiki tutakuwa na Shughuli mbalimbali hadi tufike katika kielele cha Tamasha la Michezo la Watu wa Chumbuni ambapo wananchi jimboni hapa watakuwa wamenufaika kwa fursa mbalimbali


Kwa upande wake Mwenyekiti wa wa CCM Mkoa wa Mjini  Unguja Talib Ali Talib amesema kuwa, tukio hilo ni ufanyaji wa Mazoezi linakwenda sambamba na utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi CCM.


"Alichikifanya Mbunge wa Jimbo wa Jimbo la chumbuni  Mhe Pondeza ni utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi ambapo imetutaaka kuwasisistiza Wananchi wetu kufanya Mazoezi ili kuimarisha Afya zao," amesema.


Aidha amepongeza Uongozi wa Jimbo hilo kwa kubuni shughuli mbalimbali ambazo zinalenga kuwaunganisha pamoja sambamba na kufungua fursa kwa Vijana.



Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI