NA MWANDISHI WETU, ZANZIBAR -MATUKIO DAIMA APP
ZAIDI ya Mabondia 14 akiwemo Karimu Mandonga na Dulla Mbabe wameendelea na ziara katika Maeneo mbalimbali Visiwani Zanzibar lengo likiwa kuhamasiha Wananchi kujitokeza kwa Wingi katika ufunguzi wa Mchezo wa ngumi za Kulipwa Agost 27 mwaka huu.
Mabondia hao wamekuwa kivutio kikubwa katika Mitaa mbalimbali Visiwani humo ambapo Usiku wa Jana walifika katika eneo maarufu la Forodhani kwa ajili ya kuhamasisha Wanachi na Kula chakula cha Jioni.
Wakizungumza na Waandishi wa Habari Wafanyabiashara katika eneo la Forodhani, wamesema kuwa Ujio wa Mabondia hao umetoa fursa za kibiashara kwao ambapo mauzo yameongezeka zaidi.
"Ukweli kuwa tumefurahi leo kwa kumuona Mandonga katika eneo la Forodhani na mauzo ya biashara kwetu leo yameongezeka hadi kufikia Milio 2 na kuendelea," wameeleza.
Aidha Wafanyabiashara hao waipongeza Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kwa kuruhusu Mchezo wa Ngumi za Kulipwa Visiwani humo kwani unatoa fursa mbalimbali za Ajira kwa Vijana.
"Ukweli kuwa Mchezo huu unatoa fursa za Ajira kwa vijana wetu pamoja n kutangaza Visiwa hivi," walieleza.
Mabondia hao wanatarajiwa kupima Afya zao kuelekea Mapambano hayo ambayo yanatarajiwa kufanyika katika katika Viwanja vya Maotsung Mjini Magharib Unguja.
0 Comments