Header Ads Widget

KANISA KATOLIKI LATOA TAMKO KUPINGA MKATABA WA BANDARI.


Na Simon Joshua - Matukio Daima App, Iringa.

Baraza la maaskofu wa Katoliki Tanzania limetoa tamko la kupinga mkataba wa usimamizi na uendelezaji wa bandari za nchi hiyo uliosainiwa kati ya serikali ya Tanzania na Dubai na kuridhiwa kupitia azimo la Bunge Juni 10 mwaka huu,kwa maelezo kuwa haukubaliki kwa watanzania wengi.


Tamko hilo kutoka kwa maaskofu 37 Wakatoliki limetangazwa kwa umma na katibu mkuu wa Baraza la Maaskofu Wakatoliki Tanzania, Padre Charles Kitima.


Padre Kitima amesema maaskofu hawaungi mkono bandari kuwekwa chini ya mwekezaji mmoja na kwamba tamko hilo la maaskofu lina lugha moja tu, nayo ni kwamba kama wananchi hawautaki mkataba, serikali iwasikilize wananchi.


Hata hivyo serikali ya Tanzania mara kadhaa imesema kupitia viongozi mbalimbali mkataba huo una tija kubwa kwa uchumi na maendeleo ya nchi hiyo.


Mjadala juu wa uwekezaji unaotarajiwa katika usimamizi wa bandari za Tanzania umedumu tangu mwanzoni mwa mwezi Juni mwaka huu huku kukiwa na mitazamo tofauti kati ya wanaounga mkono na wanaopinga.

Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI