Header Ads Widget

VUNJA BEI WADHAMINI LIGI YA WILAYA IRINGA MJINI,MATUKIO DAIMA MEDIA WAONGEZEKA NGUVU

TIMU 10 kushiriki ligi ya Wilaya ya Iringa Mjini inayotaraji kuanza kesho katika viwanja vya Shule ya Msingi Mlandege Mjini hapa.


Mwenyekiti wa chama cha Soka Wilaya ya Iringa Mjini Joel Musiba akizungumza Jana wakati wa hafla fupi ya mdhamini wa ligi hiyo kukabidhi vifaa vya michezo kwa timu shiriki ,alisema mwitikio wa timu umekuwa mkubwa na wanaamini kupata timu Bora itakayowakilisha Wilaya kwenye ligi ya mkoa.


Musiba alisema pamoja na mafanikio ya kupata mdhamini kampuni ya Vuja Bei ambayo imejitolea vifaa vya michezo kwa maana ya jezi na mipira kwa timu shiriki ila bado wanaomba Wadau wengine kujitokeza kudhamini ligi hiyo.


Alisema mdhamini mkuu wa ligi hiyo  iliyopewa jina la Fadhil Ngajilo Manispaa Cup 2023 ni kampuni ya Vuja Bei .


Pamoja na kupongeza kampuni ya Vuja Bei kwa kujitolea vifaa vya michezo na kudhamini ligi hiyo kwa kutoa kiasi cha tsh milioni 2 pamoja na zawadi ya kombe na Ng'ombe kwa Mahindi wa kwanza pia alipongeza kampuni ya Matukio Daima Media kwa kujitolea zawadi ya jezi seti Moja kwa timu itakayoonesha nidham kwenye ligi hiyo .



Huku akiomba Wadau wengine kuendelea kujitokeza kuongeza udhamini zaidi .


Kwa upande wake mdhamini mkuu wa ligi hiyo kupitia kampuni ya Vuja Bei Fadhil Ngajilo  alisema kampuni yake imeendelea kudhamini ligi hiyo kwa mwaka wa pili mfululizo Sasa na itaendelea kudhamini .


Alisema mwakani wamepanga kuongeza udhamini zaidi na ikiwezekaza ligi ya Iringa Mjini iwe Bora kuliko ligi yoyote ya ngazi ya Wilaya Tanzania na nje ya Tanzania .


Ngajilo alisema mkoa wa Iringa kupitia ligi hiyo ya Wilaya umeandika histori Kubwa katika Soka la Tanzania kwa kutoa mchezaji mahili anayechezea timu ya Yanga Sc Clement Mzinze  ambae ni matunda ya Iringa.


Hivyo alisema Ili kuendelea kuwa jiko la wachezaji Bora zaidi udhamini utaongezwa na ikiwezekana Soka litaanza kuibuliwa ngazi za chini zaidi .


Ngajilo ambae pia ni Mwenyekiti wa jumuiya ya wazazi CCM mkoa wa Iringa alisema michezo ni utekelezaji wa Ilani ya CCM hivyo sanjari na ligi hiyo kampuni yake inakuja na uhamasishaji wa michezo yote ndani ya mkoa wa Iringa .


Huku kwa upande wake mkurugenzi wa matukio Daima Media Francis Godwin pamoja na kujitolea zawadi ya timu yenye nidhamu pia alisema anakusudia kuongeza zawadi kwenye ligi hiyo .


Pia alisema  Matukio Daima Media kwa kushirikiana na chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) wanataraji kuendesha mdahalo mkubwa wa michezo lengo likiwa kuhamasisha Wadau Kuunga Mkono michezo Ili kuurejesha mkoa wa Iringa ligi kuu Tanzania bara .



Katibu wa chama cha Soka Wilaya ya Iringa Mjini Yahaya Mpelembwa alisema timu zote zibazoshiriki ligi hiyo zinapaswa kuzingatia Nidhamu .


Alisema tayari makundi yamepangwa  kwa kundi A kuwa na timu ya Makorongoni FC,Ruaha Academy ,itamba Fc,Donbosco Fc na Mshindo Fc .


Wakati kundi B ni timu ya African Wonderer's ,City Boys ,Streto Fc .Under The Tree na VETA Fc 






Post a Comment

0 Comments



MAGAZETI



NAMBA ZA HUDUMA YA USAFIRI WA KUKODI