NA MATUKIO DAIMA APP,ZANZIBAR
BAADA ya Zanzibar kuruhusu Mchezo wa Ngumu, Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBRC imetoa Mafunzo na Uzoefu wa namba bora ya kuendesha Mchezo wa huo kwa Wajumbe wa Kamsheni ya Ngumi za Kulipwa Zanzibar pamoja na Wadau mbalimbali.
Mafunzo hayo yalifanyika katika Ukumbi wa Hotel ya Serena Shangani Mjini Unguja kuelekea ufunguzi wa Mchezo wa Ngumi VIsiwani humo Agost 27 mwaka huu katika Viwanja vya Maotsung.
Akizungumza na Waandishi wa Habari Rais wa Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania TPBRC Chaurembo Palaso amesema kuwa Mafunzo hayo yamejumuisha taratibu zote ambazo zinatakiwa kufatwa kabla, wakatii na baada ya Mchezo wa Ngumi.
"Leo hapa tumetoa Mafunzo kwa Ndugu zetu kamisheni ya Ngumi za Kulipwa Zanzibar ambapo tumewaeleza mambo muhimu ambayo ya kuzingatia kabla na baada ya mchezo," ameesema.
Ameeleza kuwa, Katika Mafunzo hayo pia wameeleza Kanuni, Sheria na Taratibu Mchezo wa Ngumi zinavyotakiwa kufatwa ili mchezo huo usilete madhara katika jamii.
"Tumebadilishana Uzoefu wa namna ya kuendesha mchezo wa ngumi ambao sasa hivi umebeba ajira nyingi sana kwa vijana wetu," ameeleza.
Kwa Upande wake, Makamu wa Rais wa Shirikisho la Ngumi za Kulipwa Zanzibar Edwin Robart ameishukuru Kamsheni ya Ngumi za Kulipwa Tanzania bara kwa kuendesha Mafunzo na kubadilishana Uzoefu wa namna ya kuendesha mchezo huo.
Akizungumzia Kuelekea Ufunguzi wa Mchezo wa Ngumi za Kulipwa Zanzibar amesema kuwa, maandalizi yamekamilika na Wananchi visiwani humo wasubiri kuona burudani ya kutosha.
"Hadi sasa Maandalizi ya Ufunguzi wa Ngumi za kulipwa yanakwenda vizuri ambapo Wapenzi wa Mchezo wa ngumi sasa wasubiri burudani kwani katika kiwanja cha Mau hapatatosha, uwanja utapambwa kwa aina yake," ameesema.
Ameeleza kuwa, Mgeni rasmi katika ufunguzi wa ngumi Zanzibar anatarajiwa kuwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Hussein Ali Mwinyi.
"Mbali na Rais katika Ufunguzi wetu wa Ngumi Zanzibar siku hiyo tutakuwa na Wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva kutoka Bara na Visiwani ambao watanogesha Mchezo huo," ameeleza.
Zaidi ya Mabondia 14 akiwemo Dulla Mbabe na Karimu Mandonga wanatarajiwa kupanga Uliongoni Agost 27 mwaka huu katika kiwanja cha Maotsung Mjini Unguja.
0 Comments